Flatnews

RONALDO Vs MESSI NDANI YA OLD TRAFFORD JUMANNE YA LEO USIKU NOVEMBER 18/2014

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo ametua kwenye ardhi ya jiji la Manchester hapo jumapili jioni mbele ya mchezo wa kesh...


3
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo ametua kwenye ardhi ya jiji la Manchester hapo jumapili jioni mbele ya mchezo wa kesho wa kimataifa wa kujipima ubavu baina ya Ureno dhidi ya Argentina, mchezo ukitarajiwa kupigwa Old Trafford.

Huu ni mchezo ambao unawakutanisha nyota wawili ambao wanatajwa kwamba huenda mmojawapo atatwaa ile tuzo ya Ballon d’Or, na hawa ni Christiano Ronaldo na Lionel Messi wakiwa wanakutana kwa mara ya 27 katika historia yao.
Akiwa amevaa kofia nyekundu ya Baseball yam kali wa zamani wa kikapu Michael Jordan inayotengenezwa na kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike, Ronaldo aliwasili jijini Manchester akiwa kivutio cha mashabiki.
1
Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Manchester United atakuwa akicheza mchezo wake wa pili uwanjani hapo, tangia alipoondoka mnamo mwaka 2009, kuelekea klabu ya Real Madrid ya Uhispania, pambano ambalo linatajwa kuwa ni baina yake yeye na Messi.
Messi atakuwa anakanyaga kwenye ardhi ya viwanja vya Uingereza kwa mara ya pili akiwa na timu yake ya taifa, ikiwa ni siku tano tu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Croatia kule Upton Park juma lililopita
Hii ni kama ilivyo kwa mshambuliaji mwingine wa nchi hiyo Carlos Tevez ambae alirejea kulikokuwa nyumbani kwake, jijini London kwenye makazi ya klabu yake ya zamani, ya West Ham United.
7
Ronaldo, alipachika bao la ushindi kwenye mchezo wa kuwania kufuzu mihuao ya fainali za Ulaya zitakazofanyika nchini Ufaransa mwaka 2016, bao ambalo lilimfanya kuweka rekodi mpya.
Mshmbuliaji huyu anakuwa amesogea mbele ya mshambuliaji wa zamani wa wa klabu za Newcastle United, AC Milan na timu ya taifa ya Denmark John Dahl Tomasson kwa mabao 23 katika hatua za kufuzu kwa michuano ya Ulaya na fainali zake.
10
Bado pia Messi hakuwa nyuma kuteka hisia za wapenzi wa soka jijini Manchester, kwani nyota huyu mwenye kipaji cha ajabu, alipigwa picha nyingi sana akiwa kwenye basi lililokuwa limebeba wachezaji wa Argentina, wakielekea kwenye viwanja vya mazoezi vya Manchester City Carrington.
Kwenye kikosi hiki cha Argentina, nyota wengi wamecheza au bado wanacheza soka la kulipwa nchini England, kama Angel Di Maria wa Man United, Javier Mascherano aliyewahi kuchea Liverpool, Carlos Teves aliyewahi kukipiga kwenye vilabu vyote viwili vya jiji la Manchester, na West Ham, na Martin Demichelis anaekipiga Man City, na hata beki majeruhi Marcos Roji anakipiga Man United.

Post a Comment

emo-but-icon

item