AJILIPUA KWA MAFUTA YA TAA KISA KUNYANYASWA NA BABU YAKE
Kijana mmoja Nicholas Mhagama (25), mkazi wa Makongo Juu Dar, juzi kati alijilipua na mafuta ya taa kisa kikidaiwa kunyanyaswa ...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/ajilipua-kwa-mafuta-ya-taa-kisa.html
Kijana mmoja
Nicholas Mhagama (25), mkazi wa Makongo Juu Dar, juzi kati alijilipua
na mafuta ya taa kisa kikidaiwa kunyanyaswa na babu yake. Tukio hilo
lilitokea eneo la Makongo Juu Makaburini usiku ambapo kijana huyo na
babu yake aliyemtaja kwa jina moja la Mhagama waligombana.
AJILIPUA KWA MAFUTA YA TAA
Baada
ya kijana huyo kuona isiwe tabu alijilipua na mafuta ya taa alipoona
maumivu yanazidi akaanza kupiga kelele za kuomba msaada ambapo
aliokolewa na kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala na baadaye kuhamishiwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya hali yake kuwa mbaya.
Waandishi walikwenda kufanya mahojiano naye hospitalini hapo ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Ndugu zangu naomba mnisaidie nipone kwani uamuzi niliouchukua haukuwa sahihi ni hasira za kilevi nilichokuwa nimekunywa.
“Yote
haya ni sababu ya manyanyaso niliyopata kutoka kwa babu yangu ambaye
alinifukuza nyumbani na kunitaka nikapange nyumba wakati nilikuwa na
matatizo ambayo alikuwa akiyajua,” alisema Mhagama.
Aliongeza:
“Niliwahi kukutwa na ajali mbaya ambayo ilisababisha niende kuishi
nyumbani kwa bibi yangu ambapo babu amekuwa kero. “Awali nilipofika
nyumbani sikumkuta babu lakini alipofika akawa kero kwangu kwani ni mtu
anayetaka nimpe hela kila kukicha, nilikuwa nikienda kuhangaika napata
elfu ishirini nampa elfu kumi na tano na mimi naweka elfu tano kwa ajili
ya kujipanga ili nikapange chumba.
ALIAMBIWA AKICHELEWA ATAFUNGIWA MLANGO
“Siku
ya tukio nilimuaga naenda kwa baba yangu mdogo kumsalimia akaniambia
nikirudi usiku nitakuta amefunga mlango nitafute pa kwenda kulala.
“Kweli,
niliporudi alianza kuninyanyasa kwa maneno, ugomvi wetu ukawa mkubwa
nikaona bora nijiondoe duniani kwani siwezi kuendelea kuishi maisha ya
manyanyaso kama haya,” alisema Nicholas kwa shida kutokana na majeraha
aliyonayo mwilini hasa usoni na mikononi.
Nicholas Mhagama akiuguza majeraha hospitalini.
Akizungumza
kwa njia ya simu bibi wa kijana huyo, Bi. Mhagama alikiri kwamba ni
kweli huyo babu ambaye yeye anamuita shemeji amekuwa akimnyanyasa sana
Nicholas. “Ni kweli amekuwa akimfukuza nyumbani hapo wakati siyo kwake
na siku ya tukio baada ya kuona ugomvi umekuwa mkubwa nilikimbilia kwa
mwanangu huko Kimara.
“Ugomvi
kati ya babu yake huyo mdogo na huyu Nicholas ulianza saa tatu usiku.
Nilipoona kero niliamua kutimkia Kimara kwa mwanangu,” alisema bibi
huyo.
SIMU YA MOTO YAPIGWA USIKU
“Ilipotimia saa nne usiku nikapigiwa simu na kufahamishwa kuwa Nicholas kajilipua kwa mafuta ya taa.
BABU ORIJINO ALISHAFARIKI
“Mume
wangu (Babu orijino) alishafariki na huyu Nicholas kweli kabisa huwa
anagombana na huyo babu ambaye ni shemeji yangu. “Kisa cha ugomvi wao
ni kumpa manyanyaso ya hali ya juu, nawaomba mumsaidie huyo kijana,
naombeni jamani,” alisema bibi huyo.
Juhudi za kumpata babu huyo anayedaiwa kumnyanyasa mjukuu wake hazikuzaa matunda.