NATESEKA..!!! NILIJUA NI MIMBA KUMBE NI UGONJWA
Flora Samweli Luvinga (24) anyesumbuliwa na uvimbe mkubwa tumboni.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/nateseka-nilijua-ni-mimba-kumbe-ni.html
Mgonjwa
huyo ambaye kuumwa kwake kumechukua muda mrefu bila mabadiliko ya kupata
nafuu, afya yake imezidi kudhoofu jambo lililomfanya mama yake mzazi
kupatwa na presha siku za hivi karibuni na kufariki dunia baada ya
kushindwa kupata fedha kwa ajili ya kumtibia.
Katika
mahojiano na mwandishi wa habari hii wiki iliyopita saa chache baada ya
kurejea jijini Dar akitokea Iringa, Flora aliyekutwa amekaa chini maeneo
ya Mwenge akipumzika kutokana na maumivu makali, alikuwa na haya ya
kusema:
Mama mmoja mkazi wa Kijiji cha Kipanga, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, Flora Samweli Luvinga (24) hali yake ipo hatari baada ya kuvimba tumbo na kumsababishia maumivi makali.“Awali nilidhani ni mimba baadaye nikajua kuwa kumbe siyo bali ni ugonjwa ambao unanipa mateso kwa muda mrefu, sasa sijui hatima ya maisha yangu hapa duniani,” alisema Flora.“Siamini kama ipo siku nitapona na kurejea hali yangu ya kawaida, hapa nilipofikia nimekata tamaa, kwani nimehangaika kwa muda mrefu katika matibabu bila kupata nafuu