TAZAMA KIJANA HUYU ANAVYOTESEKA
Sadick Suleiman akionyesha sehemu ya mguu wake uliokatwa.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/tazama-kijana-huyu-anavyoteseka.html
Akizungumza
na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa Hospitali ya Ocean
Road, Sadick alisema mguu wake ulikatwa kwa mara ya kwanza baada ya
kuungua moto mwili mzima alipokuwa amekwenda kuvuna korosho.
Kijana
mmoja Sadick Suleiman (24) (pichani), mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar
es Salaam amesema kuwa madaktari wanataka kuukata mguu wake kwa mara ya
tatu baada ya oparesheni mbili kufanyika pasipo mafanikio.“Nakumbuka
nikiwa darasa la nne, nikiwa na watoto wenzangu tulikwenda kuokota
korosho shambani Mtwara vijijini nilikokuwa nikiishi
na wazazi wangu, huko kuna kawaida ya watu kuandaa mashamba yao kwa kuyachoma moto.
na wazazi wangu, huko kuna kawaida ya watu kuandaa mashamba yao kwa kuyachoma moto.
“Sasa
mimi na mwenzangu ambao tulikuwa wakubwa tukiwa hatujui nini
kinachoendelea tulipanda juu ya mti kwa ajili ya kuangua korosho huku
wenzetu wakiwa chini wanasubiri kuokota, tukiwa juu tukaona moto unawaka
unakuja tulipokuwa lakini kabla hatujashuka chini, ukatuzingira,”
alisema Sadick.
Aliongeza kuwa wenzao waliokuwa chini walifanikiwa kukimbia wao wakiwa juu ya mti, uliwakuta na kila walipojaribu kushuka ndivyo ulivyozidi wakapanda zaidi juu ya mti lakini mwisho walizidiwa na kuamua kujitosa kwenye moto ambapo yeye aliungua sehemu kubwa ya mwili na mwenzake aliungua mwili mzima ikiwa ni pamoja na kichwani
