MKUSANYIKO WA U12 DAR ES SALAAM
Watoto wenye umri chini ya miaka 12 wa Mkoa wa Dar es Salaam wanakusanyika kesho Jumamosi (Novemba 22 mwaka huu) asubuhi kwenye U...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/mkusanyiko-wa-u12-dar-es-salaam.html

Watoto
wenye umri chini ya miaka 12 wa Mkoa wa Dar es Salaam wanakusanyika
kesho Jumamosi (Novemba 22 mwaka huu) asubuhi kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume kwa ajili ya kusaka kombaini ya mkoa.
Mkusanyiko
wa kusaka kombaini hiyo kwa ajili ya timu itakayoshiriki mashindano ya
Taifa yatakayofanyika mwishoni mwa mwezi ujao uko chini ya Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA).
Wachezaji
hao wataanza kujaribiwa saa 1 hadi saa 5 asubuhi. Mashindano ya Taifa
yatafanyika jijini Mwanza kuanzia Desemba 28 mwaka huu.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)