JOKATE, GAETANO KATIKA MAISHA SHOW
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/jokate-gaetano-katika-maisha-show.html
Dar
es Salaam. Mbunifu wa mitindo na muigizaji wa filamu nchini, mrembo
Jokate Mwegelo kwa kushirikiana na mshiriki maarufu wa Big Brother
Africa, Mganda Gaetano Kagwa wameteuliwa kuendesha kipindi kipya cha
Maisha kijulikanacho kwa jina la “Beat the Challenge” kupitia M-Net East
Africa.
Kipindi
kitashindanisha familia mbalimbali katika nchi za Tanzania, Kenya na
Uganda na mshindi atapewa gari jipya kabisa kutoka kwa waandaaji.
Katika mashindano hayo, kila familia inatakiwa kuwa na watu wanne ambao
ni Baba, Mama na watoto wawili wenye umri kati ya miaka 12 na 17.
Familia
hizo zitashinda katika kutatua changamoto mbalimbali zitakazowasilishwa
na waandaaji na kila familia itakuwa na jukumu la kutatua hiz
changamoto kwaa kutumia nguvu kuliko ufahamu wa akili.
Akizungumza
jana, Jokate alisema kuwa amejisikia faraja kubwa kupewa nafasi hiyo
ambayo itampa uzoefu zaidi katika fani ya utangazaji na kujipanua
kimawazo.
Jokate
ambaye pia ni Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006 alisema kuwa
anajisikia faraja kubwa kwa kuzidi kuongeza wigo wa mawasiliano kwani
hii si mara yake ya kwanza kuendesha vipindi katika televisheni baada ya
kutamba katika kipindi cha Chaneli O.
“Kama
nilivyosema, nataka kuishi kwa kutegemea vipaji vyangu na wala si
vinginevyo, nimeanza katika urembo, nikaja katika ubinifu na
uanaminitindo, MC, muigizaji wa filamu na sasa mtangazaji, kote huko
nimefanikiwa, ni faraja kubwa kwangu,” alisema Jokate.
Alisema
kuwa anashukuru kuona kuwa filamu yake ya Mikono Salama kwa sasa
inatamba sana na inamuongezea sifa kubwa katika fani hiyo. “Hata kidoti
Fashion nayo inatamba, hivyo kwa nashukuru Mungu kwa kuniwezesha,”
alisema.
Kwa
upande wa Tanzania, utafutaji wa washiriki utafanyika Jumamosi Novemba
22), New Africa Hotel, wakati Uganda watafanyia kwenye hotel ya Silver
Springs, Kampala na Kenya kwenye studio za Supersport zilizopo katika
Barabara ya Jamhuri.
Kipindi cha kwanza kitarushwa Desemba 13 kupitia chaneli ya Maisha Magic 161 kuanzia saa 2.30 usiku kwa mujibu wa Jokate.
