‘Maximo sajili ‘Domayo’ mpya’
Yanga imewapoteza viungo wake wawili wakabaji msimu huu Frank Domayo na Athuman Idd.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/maximo-sajili-domayo-mpya.html
Yanga imewapoteza viungo wake wawili wakabaji msimu huu Frank Domayo na Athuman Idd.
Dar es Salaam. Nyota wa zamani
wa Yanga na Taifa Stars, Ally Yusuph ‘Tigana’ amemshauri kocha Marcio
Maximo kumsajili kiungo mwenye uwezo wa Frank Domayo kipindi hiki cha
usajili wa dirisha dogo.
Tigana aliliambia gazeti hili jana kuwa Yanga
inahitaji kusajili kiungo mkabaji, nafasi ambayo imeonekana kupwaya
tangu kuondoka kwa Domayo aliyejiunga na Azam msimu uliopita na sasa
nafasi hiyo anacheza Mbuyu Twite.
“Twite alihamishwa kutoka beki na kucheza nafasi
hiyo ambayo bado haimudu vizuri, hivyo kusababisha pengo la Domayo
kuendelea kuonekana, kama kweli Yanga inahitaji kurejea kwa kasi, kocha
Maximo akubali kusajili kiungo mkabaji kipindi hiki cha dirisha dogo,”
alisema Tigana.
Alisema Maximo akubali au akatae, lakini Yanga
inahitaji kuwa na mchezaji atakayeziba pengo la Domayo na kusisitiza
kuwa timu hiyo itakuwa tishio endapo itasajili kiungo mkabaji mwenye
kiwango atakayeisaidia timu mara ligi itakapoendelea Desemba 26.
Alisema upande wa mabeki kikosi hicho kiko vizuri
sambamba na safu yake ya ushambuliaji ambayo alidai ina safu nzuri ya
ushambuliaji.
“Tatizo la ushambuliaji, Yanga inakosa mtu wa
kuwalisha mipira, Kiiza (Hamis), Tegete (Jeryson) na Bahanuzi (Said), ni
washambuliaji wazuri, sasa hivi wanaonekana hawafanyi kazi sababu
hawana mtu wa kuwapa mipira ya kufunga, lakini ni wazuri, hata na Jaja
anayepewa nafasi na kocha,” alisema.
Naye mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Iddi Moshi
‘Mnyamwezi’ alisema wachezaji wengi wanaosajiliwa kwa bei mbaya kwa sasa
si bora kama waliokuwa wanasajiliwa kwa bei mbaya miaka ya nyuma.
Moshi alisema: “Soka la sasa maneno na ujanja mwingi, zamani wachezaji walisajiliwa kwa ubora unaoonekana.
Tazama leo hii mchezaji anasajiliwa kwa
Sh20milioni hadi Sh30 milioni, lakini kazi yake haionekani, zaidi
utasikia kacheza mzunguko mmoja wa ligi (michezo 13) katangazwa
kutimuliwa au kawekwa benchi.
“Wakati wa nyuma, mchezaji wa kiwango cha juu
alisajiliwa Sh3 milioni hadi 5, lakini kazi yake hauwezi kuifananisha
na wachezaji wa sasa. Wengi wao sasa wanasajiliwa kisiasa bila ya
kuangalia masilahi ya timu.