MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AENDELEA NA ZIARA YAKE KATIKA KISIWA CHA HAINAN
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/makamu-wa-pili-wa-rais-zanzibar.html

Makamu wa
Rais wa Kiwanda cha Dawa za Binaadamu cha Shuangcheng Bwana Jianlin
Yuan akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na
Ujumbe wake wakati walipotembelea kiwanda hicho wakiwa katika ziara ya
Kiserikali Katika Jimbo la Kisiwa cha Hainan.

Ujumbe wa
Zanzibar Ukiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif
ukifanya mazungumzo na Ujumbe wa Makampuni ya uwekezaji vitega uchumi
katika Jimbo la Hainan ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Nyumba na Maendeleo ya Miji na Vijiji ya Hainan.

Balozi
Seif na Ujumbe wake wakiwa katika kikao cha pamoja cha ushirikiano kati
ya Zanzibar na Uongozi wa Manispaa ya Mji wa Haikou ukiongozwa na Meya
wa Mji Huo Mstahiki NI Qiang.

Mwenyekiti
wa Kiwanda cha kusindika bidhaa za nazi pamoja na matunda kiliopo
Haikuu Bwana Huang Chunguang akimfahamisha Balozi Seif na Ujumbe juhudi
zinazochukuliwa na Kiwanda hicho katika kulitumia vyema zao la nazi.
Kushoto ya Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi na Kulia yake ni
Waziri wa Ardhi Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban na Waziri wa Habari Mh.
Sai Ali Mbarouk. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.