Tazama picha 7 za Majeruhi wa ajali ya gari la Mafuta iyotokea Mbagala jiji Dar es Salaam
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/tazama-picha-7-za-majeruhi-wa-ajali-ya.html
MAJERUHI 9
kati ya 15 waliofikishwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya
kuungua na moto uliosababishwa na kuungua kwa lori la mafuta huko
Mbagala jijini Dar es Salaam Oktoba 15 mwaka huu, wanaendelea na
matibabu huku hali zao zikiwa bado mbaya.
Kamera
yetu ilifika katika hospitali hiyo na kuwakuta wagonjwa hao wakiwa
wamelazwa katika wodi namba 23 iliyopo katika jengo la Sewahaji na Afisa
Uhusiano msaidizi wa Muhimbili, Doris Ihenga alisema majeruhi sita
waliokuja pamoja nao, wamefariki dunia.
Alisema
majeruhi wawili kati ya tisa waliolazwa, hali zao ni mbaya zaidi ambao
aliwataja majina yao kuwa ni Mathayo Danie (21) na Hamis Ally (35).
Wengine
waliolazwa kwa kuunguzwa na moto huo wakati wakijaribu kuchota mafuta
yaliyomwagika kutoka kwenye tenki la gari lililoanguka ni Abbas Mohamed
(25), Hamis Kambi (25) Idd Said (30) Mathayo Daniel (21) Hamis Ally (35)
Ibrahimu Hamis (26) Maganga Mgombele (38) na Shabaki Martin.





