Flatnews

MISS TANZANIA 2014 SITTI MTEMVU ANA MIAKA 23 NA SIO 18





Katibu wa kamati ya Miss Tanzania Bosco Majaliwa amesema kuwa mshindi wa Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu amezaliwa mei 31 mwaka 1991 na umri wake sahihi ni miaka 23 na sio miaka 18 kama ilivyozagaa sehemu mbalimbali.

Katibu huyo aliongeza kuwa Sitti ana shahada ya ya uhusiano wa kimataifa na alimaliza masomo yake Desemba mwaka jana katika chuo kikuu cha North Texas kilichoko kwenye jiji la Dallas nchini Marekani.

Sitti Mtemvu bado hajasoma ngazi ya shahada ya uzamili (Masters) kwa sasa ila anatarajiwa kwenda kusoma ngazi hiyo huko nchini Marekani.

Hebu Nipe Mtazamo Wako Juu ya Hili kwa Kuzitazama Vizuri Picha Hizi na Ukilinganisha na Maelezo ya Huyo Katibu...

Post a Comment

emo-but-icon

item