Flatnews

Timu ya taifa ya Algeria ndiyo timu ya kwanza kujikatia tiketi AFCON 2015




Timu ya taifa ya Algeria ndiyo timu ya kwanza kujikatia tikiti ya kushiriki dimba la kombe la Afrika hapo Januari mwaka ujao baada ya kuinyuka timu ya taifa ya Malawi mabao 3-0.
Bao la kwanza lilifungwa baada ya dakika moja tangu mechi kuanza pale mchezaji Yacine Brahimi alipopata pasi safi kutoka kwa Islam Slimani pembeni mwa uwanja na kuvurumisha mkiki mkali ulioenda juu juu nakutingisha wavu.
Riyad Mahrez anayeichezea klabu ya Leicester city katika ligi ya Uingereza, aliongeza bao la pila katika kipindi cha pili .
Hii ni baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Sofiane Feghouli na kufunga kwa urahisi kabisa.
Mahrez aliendelea kung'ara na baadaye kutoa pasi safi ya juu iliyokamilishwa na kichwa na Slimani na kumuacha mlinda lango hoi na kufunga bao la tatu na la mwisho huku wakiisaidia Algeria kujipatia nafasi ya kushiriki dimba la kombe la taifa bingwa Afrika.

Post a Comment

emo-but-icon

item