MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA WAZIDI KUCHARUKA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KUELEKEA MECHI YA J'MOSI, NI VIJEMBE KWA KWENDA MBELE.
Maneno yanayo onekana katika picha ya basi la simba "KILIMO KWANZA" na "BUNJU" ni maneo ambayo hayapo katika ma...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/mashabiki-wa-simba-na-yanga-wazidi.html
![]() |
| Maneno
yanayo onekana katika picha ya basi la simba "KILIMO KWANZA" na
"BUNJU" ni maneo ambayo hayapo katika mabasi halisi ya Simba Sc. |
Amini
usiamini mechi ya Simba na Yanga (Dar Derby), ni mchezo wenye hisia
kali sana kwa mashabiki wa timu hizi mbili, tofauti na timu hizi
zinapocheza na timu zingine.
Nimekuwa
nikiwafuatilia mashabiki wa timu hizi mbili kwa ukaribu katika mitandao
ya kijamii hususani Face book, ndipo nikagundua hali imefikia patamu
sasa kwani licha ya mashabiki hawa "Simba vs Yanga" kutumia misemo
mbalimbali ya kukejeliani, wameona hiyo haitoshi na sasa wameanza
kwenda mbali zaidi kwa kutumia ubunifu wa kuhariri picha (picture
editing) ambazo hurushwa katika mitandao ya kijamii kila mmoja
akijitamba na timu yake.
Kwa
sasa Simba Sc klabu bado ipo Afrika ya kusini ikijiwinda na mchezo huo
wa watani wa jadi ambao utafanyika siku ya Juma mosi Oct 18, 2014 katika
uwanja wa taifa Dar es salaam, wakati huo huo Yanga Sc klabu nao wapo
hahapa mjini maeneo ya Boko ambapo hufanya mazoezi yao kila siku katika
uwanja wa Boko Veterans.

