KESI YA PISTORIUS, BINAMU APASUA JIPU MAHAKAMANI
Mwanariadha Oscar Pistorius kesi yake kusikilizwa tena kesho.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/kesi-ya-pistorius-binamu-apasua-jipu.html
Kesi inayomkabili Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius imeendelea siku ya leo ambapo binamu yake marehemu Reeva ameamua kupasua jipu mahakamani hapo nchini Afrika Kusini.
Aidha, Binamu huyo ambaye ni Kim Martin ameiambia mahakama mjini Pretoria Afrika Kusini kuwa Mwanariadha Pistorius anapaswa kupewa adhabu kali kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Upande wa utetezi , unasema kuwa Pistorius anapaswa kupewa kifungo cha nyumbani na kuhudumia jamii kwa kosa lake , pendekzo ambalo kingozi wa mashitaka Garrie Nel ameelezea kushutushwa nalo.
Nao Upande wa mashitaka unasisitiza Pistorius apewe kifungo jela akisema kitendo chake kimesababisha huzuni na kadhia kubwa kwa familia.
Pistorius alipatikana na kosa la mauaji bila kukusudia mwezi jana na huenda akakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 15 jela, lakini jaji anaweza kumpa kifungo cha nje au hata kumtoza faini.
Katika hatua nyingine Jaji, Thokozile Masipa, ameahirisha vikao vya mahakama hiyo hadi siku ya Ijumaa asubuhi.
