Flatnews

INSPECTOR HAROUN KUJA NA VIDEO MBILI

Msanii mkongwe nchini, Inspector Haroun


INSPECTOR
Msanii mkongwe nchini, Inspector Haroun
Msanii mkongwe nchinialiyewahi kutamba kwa wimbo wake ‘Asali wa Moyo’, Inspector Haroun anatarajia kuachia video mbili kwa mpigo ambazo zitafanyiwa final editing nchini Japan hivi karibuni.
Inspector amesema kuwa video hizo zitadhihirisha kuwa si kweli kwamba wasanii wakongwe hawataki kufanya video za gharama kubwa kwani katika kukabili soko la muziki la sasa ni lazima video iwe na kiwango cha juu na sio ubabaishaji ila kitu cha msingi ni kuwaambia ukweli mashabiki wa muziki nchini.
Katika hatua nyingine msanii huyo amesema kuwa ameamua kutuma video hizo nchini japan kwa ajili ya final editing ili apate picha zenye kiwango kinachotakiwa katika soko la kimataifa japo hakutaka kuzungumzia kiasi cha fedha kilichotumika katika utayarishaji wa video hizo.

Post a Comment

emo-but-icon

item