Flatnews

CHADEMA KUANZA KAMPENI YA KUIKATAA KATIBA KESHO

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza jambo katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es salaam.


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza jambo katika kikao hicho.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza jambo katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es salaam.
Wananchama waliohudhuria kikao hicho
Wananchama waliohudhuria kikao hicho.
Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kinatarajia  kuanza kesho mchakato wa kuzunguka nchi nzima kuwaelimisha wananchi waipigie kura ya hapana katiba iliyopendekezwa. Hatua hiyo  imebainishwa  kupitia  kikao cha  kamati  cha Chama cha Maendeleo  na Demokrasia  (Chadema) iliyofikia tamati  leo jijini Dares salaam.
Kwa mujibu wa Mwanasheria wa Chama hicho Tundu Lissu amesema kwamba  mchakato wa kuzunguka nchi nzima kuwaelimisha wananchi waikatae katiba iliyopendekezwa umegawanyika katika makundi matatu ambayo  ni kundi la Kanda ya Ziwa litakalozunguka kwa  siku 20, Kundi ka Baraza la Vijana na kundi la mwisho ni kundi la Uongozi wa juu wa chama hicho.
Kuhusu suala la daftari la kupiga kura, Mbowe amesema daftari hilo linapaswa kuboreshwa kwa kuwa kuna idadi kubwa ya wananchi  hawakuandikishwa,  hivyo   kwenye  uchaguzi mkuu   ujao  watakosa haki yao ya kupiga kura.
Katika hatua nyingine serikali imetoa taarifa ya kuandaa utaratibu wa kupiga kura ya maoni ambapo unatarajiwa kufanyika ifikapo mwakani. Jambo lolote linaweza kutokea kwa sababu wananchi ndio waamuzi wakuu wa katiba iliyopendekezwa.
BOFYA HAPA 

Post a Comment

emo-but-icon

item