Flatnews

LOPEZ: SITAKI BOYFRIEND WALA MUME TENA


Jennifer Lopez
Nyota na mkongwe wa muziki kutoka nchini Marekani, Jennifer Lopez amesema kuwa kwa sasa hataki tena kuwa na mahusiano yoyote ya kimapenzi na mwanaume yeyote kwani muda na upendo wake ameuhamishia kwa watoto wake mapacha Max na Emme wenye miaka 6.
Jennifer aliyewahi kuwa na uhusiano na rapa tajili duniani Diddy Dirty Money zamani Puff Daddy na kuolewa na mkongwe Marc Anthony na kupata watoto wawili mapacha amesema kuwa sasa ni muda wake kuonesha ni jinsi gani anawapenda wanae na si muda wa kuhangaika na wanaume.
Jennifer amesema kuwa kipaumbele chake kwa sasa ni kuwa mama bora japo marafiki zake wanamshauri apate mtu aishi nae kama mume au boyfriend.

Post a Comment

emo-but-icon

item