Flatnews

DAVIDO, WIZKID KUCHUANA BEFFTA UK AWARDS 2014

Davido na Wizkid


Davido na Wizkid
Davido na Wizkid
Wasanii nyota kutoka nchini Nigeria, Davido na Wizkid wametajwa kuwania tuzo za ‘Black Entertainment, Film, Fashion, Television and Arts’ (BEFFTA UK AWARDS 2014) za nchini Uingereza.
Wapinzani hao wanawania tuzo hizo kupitia kipengele kimoja cha ‘Best International African Act’ wakichuana na wasanii wengine kama Sarkodie, P-Square, Timaya, Olamide, Eddy Kenzo, Wande Coal, Awilo Longomba, Tiwa Savage, Emma Nyra, Burna Boy,Nathalie Makoma, Jose Chameleone na Sauti Sol wa Kenya.
Katika hatua nyingine upigaji kura utafanyika ndani ya siku 8 na ulianza rasmi October 15 na unatarajiwa kukamilika October 22 ambapo tuzo hizo zitatolewa October 24 na 25 jijini London.

Post a Comment

emo-but-icon

item