HII KALI REFA NICOLAS AMLIMA KADI NYEKUNDU CAVANI KISA KUSHANGILIA KWA STAILI YA MTUTU WA BUNDUKI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/hii-kali-refa-nicolas-amlima-kadi.html
France.
Mwanasoka
huyo wa kimataifa wa Ufaransa alipewa kadi hiyo na refa Nicolas
Rainville, baada ya kushangilia bao la mwisho la timu yake kwa ishara ya
kupiga bunduki, staili maarufu kwa klabu ya Arsenal ya England.
Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi ameponda maamuzi hayo ya utata akisema kwamba kama adhabu zitatolewa kwa ushangiliaji wa
aina hiyo, ni mbaya kwa soka ya Ufaransa.
Mabao
ya PSG yalifungwa na Cabaye dakika ya 28, Maxwell dakika ya 33 na
Cavani dakika ya 55, wakati Lens pia ilipoteza wachezaji wawili
waliotelewa kwa kadi nyekundu, Gbamin na Le Moigne, huku bao lao la
kufutia machozi likifungwa ma Coulibaly dakika ya
10.