BAADA YA AMBER ROSE SASA NI SARA DAJSTANI
Wiz Khalifa na Amber Rose enzi za uhusiano wao
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/baada-ya-amber-rose-sasa-ni-sara.html
Baada ya ndoa ya rapa Wiz Khalifa na Amber Rose kuvunjika hivi
karibuni ikiwa imedumu kwa miezi 14 tu huku wakimuacha mtoto wao
Sebastian mwenye umri wa miezi 20 akiwa katika malezi ya upande mmoja,
inasemekana kuwa Wiz Khalifa anatoka na mwanamitindo na model Sara
Dajstani.
Wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja katika sehemu mbalimbali za starehe nchini Marekani ambapo Jumanne ya wiki hii wameonekana maeneo ya Hollywood wakila bata japo ilikuwa ngumu kupata picha yao wakiwa pamoja.
Wiz na Sara walionekana wakiingia pamoja na kuondoka pamoja katika kiwanja hicho kitu kinachowafanya watu wadai kuwa Wiz na Amber Rose wanafanya mchezo wa kuoneshana kuwa wapo na nani kwa sasa.