Young Killer arekodi wimbo na Fid Q , aupa jina la tarehe yao ya kuzaliwa ’13’, umefanywa na maproducer 4 akiwemo Majani
Rapper kutoka Rock City, Young killer Msodoki wiki hii amerekodi wimbo mpya ambao amemshirikisha kaka yake rapper Fareed Kubanda aka Fi...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/young-killer-arekodi-wimbo-na-fid-q.html
Rapper
kutoka Rock City, Young killer Msodoki wiki hii amerekodi wimbo mpya
ambao amemshirikisha kaka yake rapper Fareed Kubanda aka Fid Q, ambaye
pia anatoka Mwanza.
Msodoki amezungumza na Bongo 5 kuhusu wimbo huo, “Ni project mpya kabisa kali naweza kusema kwasababu imekutanisha wakali wawili halafu kutoka mji mmoja”, alisema Killer.
Amesema
kuwa jina la wimbo huo ’13’, limetokana na tarehe ya kuzaliwa yeye na
Fid ambao wanashare tarehe moja ya kuzaliwa lakini mwezi na mwaka
tofauti.
“Hii
ngoma inaitwa ‘Kumi na Tatu’ (13), kumi na tatu ni tarehe ila
hatujaamua kuiita tarehe 13 ila inaitwa 13, kwasababu tarehe 13 ni siku
ambayo kazaliwa Fid Q na ndio siku ambayo nimezaliwa mimi kwahiyo wote
ni 13, kwahiyo ngoma tumeamua tuiite 13.” Fid amezaliwa August 13 huku Msodoki April 13.
Ameendelea kusema kuwa ‘Kumi na Tatu’ imefanywa na maproducer wanne akiwemo mkongwe P-Funk Majani.
“Ni
ngoma ambayo imefanyika Bongo Records producer akiwa ni Majani, ila
beats wakiwa wamepiga watu tofauti tofauti, kuna Lollipop, kuna Amiga
Tyga, kuna Palla Midundo. Hawa ni watu watatu ambao kila producer
nilikuwa nikimpelekea namwambia afanye kitu kimoja ambacho yeye anaweza
akafanya…ndio nikafanya kitu kimoja ambacho ambayo vocal ndio akafanya
Majani”.
Young Killer alishare picha IG wakiwa studio na kuandika:
“#ILIKUWA SIKU YA FURAHA SANA JANA BAADA YA KUKAMILISHA NDOTO YANGU YA KUFANYA KAZI NA (p.funky MAJANI) ha ha ha
RAHA SANA @majani187 (13) kumi na tatu ). Ha ha ha imenipa wakati mzuri xana wa kutabasamu.. Ha ha ha ha”
Mashabiki wa Msodoki wakae mkao wa kula sababu collabo hiyo inatarajiwa kutoka siku si nyingi.
“Kutoka
nadhani inaweza ikawa kama wiki moja na nusu mbele itakuwa imetoka
kwasababu hapa video ya ‘Umebadilika’ muda si mrefu nitai release,
kwahiyo nitaipa gap kidogo kama wiki moja na nusu wiki mbili flani ntai
release ngoma”.
Credit Bongo5