Mwanzilishi wa Kampuni ya 'Apple' Aliwazuia Watoto wake Kutumia iPad, iPhone na iPod, Fahamu Sababu
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/mwanzilishi-wa-kampuni-ya-apple.html
Bidhaa
za kampuni ya Apple zina mashabiki na wateja wengi duniani, hii
inathibitishwa na foleni kubwa ya watu waliojitokeza kwenye vituo
mbalimbali duniani kununua toleo jipya la iPhone6.
Tumesikia
watu wakiachana ama familia zikitengana kwa sababu tu baba ameshindwa
kununua bidhaa za kielekroniki za kampuni ya Apple. Mwaka jana familia
moja nchini China iliwauza watoto wao ili kupata pesa ya kununua
iPhone5.
Kwa
kuzingatia hayo, huenda ukadhani watoto wa mwanzilishi wa kampuni ya
Apple na mgunduzi wa bidhaa hizo, Steve Jobs wanafaidi zaidi bidhaa
hizo.
Na
huenda ukadhani hata kuta za nyumba yao zingeweza kuwa za mfumo wa simu
za kisasa za kupangusa ‘Screen Touch’ na mawasiliano ya hali ya juu
ndani ya nyumba hiyo kwa mfumo huo.
Lakini
ukweli ni kwamba, marehemu Steve Jobs hakuwaruhusu hata kidogo watoto
wake kutumia iPhones, iPods wala iPads nyumbani kwake.
Katika
article iliyoandikwa na New York Times wiki hii, mwandishi wa habari
Nick Bilton ameeleza jinsi ambavyo alishangaa majibu ya Steve Jobs
alipomuuliza jinsi ambavyo watoto wake wanapenda bidhaa za kampuni hiyo.
“Hawajawahi kutumia kabisa. Tunadhibiti kiasi ambacho watoto wetu wanatumia teknolojia nyumbani.” Alijibu Steve Jobs.
Nae
mwandishi maalum wa Steve Jobs, Walter Isaacson ambaye alikuwa akitumia
muda mwingi nyumbani kwa boss wake huyo alithibitisha kuwa maoengezi ya
uso kwa uso yalitawala katika nyumba hiyo.
“Kila jioni Steve alikuwa akipata chakula cha usiku na familia yake kwenye meza kubwa jikoni, wakijadili vitabu na historia na vitu vingine vingi. Hakuna mtu aliyekuwa na iPad au computer. Watoto hawakuonekana kuwa addicted hata kidogo na vifaa hivyo.” Alieleza Isaacson.
Utafiti
uliofanywa katika eneo la Chuo Kikuu cha California, Los Angeles na
kuchapishwa hivi karibuni unaonesha kuwa siku chache baada ya kuzuia
watoto kutumia vifaa vya kieletroniki vya simu, ufaulu wa watoto katika
masomo ulipanda ghafla.
Utafiti
unaonesha kuwa kwa wastani watoto nchini Marekani hutumia zaidi ya saa
saba na nusu kwa siku katika matumizi ya simu za kupangusa na vifaa
vingine vya kielekroniki kama iPads, iPod n.k.
Uamuzi ni wako, kumnunulia mwanao vifaa vya hivyo au kumuweka mbali na mapinduzi hayo ya kiteknolojia.