Kada Mzalendo Loveness Mamuya na Mrejesho wa Kwanini Usiku wa Jakaya ni Kitu cha Kujivunia Daima
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/kada-mzalendo-loveness-mamuya-na.html
1. UTANGULIZI
Binadamu
hakuumbwa katika ombwe, ameumbwa akiwa katika dimbwi la majukumu, kwake
binafsi, familia, jamii na dunia kwa ujumla. Wachache sana wanaoweza
kupitia ngazi zote za uwajibikaji huu. Katika hao wachache, hatutasita
kumtaja Jakaya Khalifan Mrisho Kikwete. Ili kujijenga vema katika
misingi ya uongozi, Jakaya Kikwete alijijenga vema katika taasisi hizi
za msingi na alipikwa vema.
Mheshimiwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni
aina ya kiongozi pekee ambaye alihudumu nafasi mbalimbali ndani ya chama
na serikali. Safari yake ya uongozi ilianzia ndani ya chama cha TANU.
Alikuwa kiongozi wa Vijana wakati wa TANU na baadaye CCM hadi kuwa
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi. Wakati wote katika nafasi zake
kwenye chama na serikali, Mh. Kikwete alihimiza maendeleo katika Jimbo
lake na watanzania kwa ujumla.
Kimsingi
amekuwa chachu ya maendeleo katika kipindi cha urais wake kuanzia mwaka
2005 hadi 2014 ambapo ameshatekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo
ambapo mingi imeshakamilika na mingine inategemewa kukamilika mwishoni
mwa mwaka 2015.
2. HISTORIA YA MAENDELEO
Kimaendeleo,
Tanzania ya mwaka 1961 si ya sasa. Tulipopata uhuru mwaka 1961,
Tanzania ilikuwa ni nchi changa ambayo haikuwa na mfumo thabiti wenye
kuleta maendeleo. Hii ni kutokana na athari tulizozipata wakati wa
ukoloni mkongwe (Classical Colonialism) na Ukoloni Mamboleo, Vita ya
Kagera na Maanguko ya kimataifa ya Uchumi. Hali hii iliathiri shughuli
za maendeleo kutokufanikiuwa kwa kiwango cha juu. Tanzania ilipitia
kipindi kigumu kiuchumi na vita mwaka 1977 mpaka 1979 ambapo ilipelekea
athari zaidi kiuchumi hadi miaka ya 1980 ambapo Tanzania ililazimika
kukaribia soko huria ili kujenga uchumi. Miaka ya 1990 mpaka miaka ya
2000 Tanzania imesonga mbele kiamendeleo kutokana na juhudi mbali mbali
marais ambao wamekuwa wakifanya katika vipindi tofauti vya uongozi wao
ambapo Nyerere kutoka 1962 mpaka 1985, Mwinyi kutoka 1985 mpaka 1995,
Mkapa kutoka mwaka 1995 mpaka 2005 na kwa sasa tuna Mh. Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alianza
uongozi kama Rais kuanzia mwaka 2005 mpaka 2015.
3. MAENDELEO WAKATI WA AWAMU YA NNE CHINI YA UONGOZI WA JAKAYA KIKWETE
Akiwa
na dhamira ya kuhakikisha kwamba kila mtanzania anapata fursa sawa
katika utumizi wa rasilimali asili na watu zilizopo ili kumjengea uwezo
kila mtanzania kufikia kiwango cha maisha bora, Mh. Kikwete alinuia
kuboresha maeneo ya msingi yatayowapeleka watanzania katika kilele cha
“MAISHA BORA”. Ili kuijenga barabara ya kuelekea katika kilele hiki,
awmu ya nne ya serikali yake ilitia mkazo katika maeneo kadhaa kama
ifuatavyo:
a) Kukuza utawala bora.
Mheshimiwa
Rais, ni dhahiri kuwa kiwango cha utawala bora katika nchi yetu
kimezidi kuimarika siku baada ya siku tena kwa ufanisi mkubwa tangu
ulipoingia madarakani. Hilo linathibitika zaidi kwa kuaangalia maeneo
mawili makubwa ambayo ni kupunguza urasimu katika shughuli mbalimbali za
kiserikali ili kurahishisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
Mashirika mbalimbali duniani yamekuwa yakitambua mchango wako na
kukuwezesha kutunukiwa nishani mbalimbali ambazo hakika ulistahili, kama
wasemavyo wahenga “ chanda chema huvikwa pete”
Kutokana
na uongozi wako mahiri, Tanzania imepata mafanikio katika nyanja za
demokrasia na utawala bora kama ambavyo Mpango wa Afrika wa Kujitathmini
katika Utawala Bora (APRM) umebainisha kwamba Tanzania ni kati ya nchi
zinazofanya vizuri kwenye eneo la utawala bora.
Tanzania
imefikia katika kuridhia na kutekeleza mchakato wa Kujitathmini katika
Utawala bora kwa nchi za Afrika (APRM) kuwa ni kuwashirikisha wananchi
kutoa maoni yao kuhusu hali ya utawala bora nchini na serikali kuruhusu
wataalamu wa utawala bora kutoka nchi wanachama kuja nchini kuhakiki
mchakato huo.
Ni
ukweli kuwa APRM ni mpango ulioasisiwa Machi 9, mwaka 2013 na wakuu wa
nchi za Umoja wa Afrika (AU) ambapo Mheshimiwa rais ulikuwa mstari wa
mbele katika kuhakikisha Tanzania inatoa fursa ya kujipima na kujua
mwenendo wa serikali na madereva wa utekelezaji (Viongozi wa serikali)
Tanzania
kwa sasa ni miongoni mwa nchi 34 kati ya 54 za AU zilizokwishajiunga na
mpango huu, ikiwa imejiunga tangu mwaka mwaka 2004.
Suala la elimu.
Elimu
ni nyenzo ya msingi katika jitihada za kujenga uchumi wa kisasa wa Taifa
linalojitegemea na kuwawezesha kiuchumi wananchi. Uchumi wa kisasa
unahitaji watenda kazi wenye maarifa yanayohusu kanuni na maarifa ya
kumudu vitendea kazi vya aina mbalimbali.
Wanafunzi
wanaojiunga na vyuo vikuu vilivyopo nchini Tanzania waliongezeka kutoka
55,296 mwaka 2005/2006 hadi 118,000mwaka 2009/2010.Idadi ya vyuo vikuu
imeongezeka kutoka vyuo vikuu 23 mwaka 2005 hadi kufikia vyuo 31 mwaka
2010.
Kuweza kujenga chuo kikuu cha Dodoma chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 40,000 kwa mwaka na kwa sasa kina wanafunzi 17,282
Wanafunzi
wanaomaliza elimu ya msingi na kuendelea na elimu ya sekondari
wameongezeka kutoka 493,636 hadi 999,070 huku idadi ya wanafunzi
wanaogharamiwa na serikali toka familia zenye kipato duni ikiongezeka
toka 16,345 hadi 58,843. Ongezeko hili ni kati ya mwaka 2005 hadi mwaka
2009. Pia Uandikishaji katika elimu ya awali umeongezeka kutoka
wanafunzi 638,591 hadi wanafunzi 889,363.
Tanzania
imeweza kupiga hatua kubwa kwenye utaoji elimu kwa wananchi wake. Kwa
kupitia(Mpango Wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi) MMEM, MMES na MEMKWA;
watoto wengi wa Kitanzania wamepata fursa ya kujiunga na elimu ya msingi
na sekondari. Hadi mwaka 2010 zaidi ya watoto milioni 8 (ambao ni zaidi
ya 90% ya uandikishaji halisi) wameandikishwa shule za msingi na zaidi
ya wanafunzi 1, 638, 699 wako sekondari.
Idadi
ya shule na walimu imeongezeka maradufu. Hadi mwaka 2010 shule za
sekondari zimeongezeka kutoka shule 937 na kufikia idadi ya 4,2663 mwaka
2010. Walimu nao wameajiriwa kwa idadi kubwa ili kusaidia mchakato wa
kuwapatia watoto elimu. Kwa mfano, hadi mwaka 2010 idadi ya walimu wa
shule za msingi na sekondari imefikia walimu 206, 3734 kutoka idadi ya
walimu 54,869 mwaka 2001. Ongezeko hili limechangiwa na ongezeko kubwa
la wanafunzi kwa kuanzia miaka ya 2001 hadi 2010.(tazama jedwali na 1).
Hii ni dhahiri kuwa fursa za elimu kwa wote zimeongezeka nchini, na
hatuna budi kuipongeza serikali chini ya Rais Jakaya Kikwete na wadau wa
elimu kwa jitihada hizo.
Mafanikio katika sekta ya Afya
Mheshimiwa
rais, tunapenda kukupongeza kwa kiasi kikubwa kwa jitihada zako katika
sekta hii muhimu katika taifa letu. Wote tunafahamu maradhi ni moja kati
ya maadui wakubwa ambao wanalisonga taifa letu toka tupate uhuru.
Ni
dhahiri kuwa tangu ulivyoingia madarakani umekuwa ukipambana kwa dhati
ili kuhakikisha mapambano juu ya maradhi yanapungua kwa kiasi kikubwa.
Wote ni mashahidi kwamba umepigania sana afya ya mama na mtoto kwa lengo
moja kuu ambalo lilikuwa ni kupunguza vifo vya kina mama wajawazito
pamoja na watoto kwani hicho kimekuwa ni kilio kikubwa na tatizo kubwa
ambalo linazikabili nchi zinazoendelea, kuna msemo usemao ukimsaidia
mwamke basi umeokoa jamii nzima, hivyo basi ni dhahiri kuwa kwa nia yako
hiyo umefanikiwa kuokoa jamii kubwa sana ya watanzaia wa kizazi
kijacho.
Mheshimiwa
Rais, umechangia kwa kiasi kikubwa kupambana na ugonjwa wa Malaria
ambao umekuwa tishio sio tu Tanzania bali hata Afrika kwa ujumla lakini
kwa jitihada zako za dhati kabisa toka moyoni ulikuwa muhamasishaji
namba moja katika kupiga vita ugonjwa huu. Ni ukweli usiopingika kampeni
mbalimbali kama vile “zinduka” na zingine ambazo zilibeba dhana ya
kuhamasisha jamii kutumia chandarua zimekuwa na mchango mkubwa sana
katika jamii yetu.
Mheshimiwa
Rais, vilevile umetoa mchango mkubwa sana katika vita dhidi ya ugonjwa
hatari kabisa wa ukimwi kwani wakati unaingia madarakani ugonjwa huu
ulikuwa ni tishio sana lakini kwa jitihada zako umefanikiwa kwa kiasi
kikubwa kupunguza maambukizi kama ambavyo takwimu za tume ya kudhibiti
UKIMWI (TACAIDS) za mwaka 2014 zinatuonesha maambukizi mapya ya Virusi
vya Ukimwi nchini yamepungua hadi kufikia asilimia 5.1 kwa mwaka
2011/2012 ambapo asilimia 6.2 ni wanawake na asilimia 3.8 ni wanaume.
Mheshimiwa
Rais, katika awamu zako mpaka sasa umejitahidi kwa kiasi kikubwa
Katika kuyaendeleza makundi mbali mbali ya kijamii,kwa namna moja ama
nyingine, na katika hilo kuna mafanikio ya moja kwa moja ambayo
yanonekana kama vile
Wanawake.
Hatua ya kurekebisha sheria zinazowabagua na
kuwadhalilisha
wanawake katika usawa na maslahi yao imetekelezwa. Sheria ya makosa ya
kujamiiana na sheria ya kuwalinda, wajane, zimerekebishwa na Sera ya
Hifadhi na Maendeleo ya Wanawake, ziliboreshwa na kusimamiwa kwa kiwango
stahiki kwa mfano uanzishwaji wa BENKI YA WANAWAKE pamoja na utoaji wa
mikopo mbalimbali mfano mkopo kwa watu wa chini maarufu kama “MABILIONI
YA JK”. Pamoja na miradi maalum wa kuinua kipato cha wanawake ili
kupunguza ajira mbaya kwa watoto umeanzishwa.
Pia
idadi ya wanawake katika nafasi mbalimbali za juu za uongozi
imeongezeka katika kipindi cha 2010-215 kwa mfano nafasi ya spika wa
Bunge ambayo kwa sasa anahodhi mwanamke mheshimiwa Anne Makinda....
takwimu zinaonyesha katika kipindi cha uongozi wako nafasi za wanawake
bungeni ni...... ambayo ni sawa na asilimia.... ukilinganisha na
mwaka....pia hata katika bunge la katiba linaloendelea idadi ya wanawake
ni... ..
Walemavu
Ili
kulinda na kusimamia haki, usawa na maendeleo ya watu wenye ulemavu,
Baraza la Taifa la Maendeleo ya Watu wenye Ulemavu, limeanzishwa chini
ya uongozi wa Afisi ya Waziri Kiongozi. Aidha, Sera ya Walemavu
imepitishwa na rasimu ya awali ya Sheria ya Walemavu imekamilika.
Hatua
za kuelimisha jamii juu ya masuala mbali mbali ya kuwaendeleza watu
wenye ulemavu, zimetekelezwa. Jumla ya watu 219 wenye ulemavu wamepatiwa
mafunzo ya uendeshaji wa biashara ndogo ndogo Unguja na Pemba pamoja na
kupatiwa mkopo wa kujiendeleza. Watu 193 wenye ulemavu wa kutosikia
(viziwi)
wamepatiwa mafunzo ya lugha ya ishara.
Miundo mbinu
Kipindi cha miaka kumi iliyopita cha 2000 – 2010 tumeshuhudia kuwepo kwa
ujenzi
mkubwa wa miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege na madaraja
nchini. Miradi yote ya ujenzi ambayo haikukamilishwa kati ya 2000 – 2005
imekamilishwa kati ya 2005 – 2010 na kuanzishwa ujenzi wa miradi mipya
kitakwimu, ujenzi wa miradi 15 kwa kiwango cha lami yenye jumla ya urefu
wa Km. 1,398.6 imekamilishwa katika kipindi cha 2005 - 2010. Aidha,
ujenzi ambao unaendelea ni wa miradi 29 ya barabara zenye jumla ya Km.
2,536.4 na wakati huo huo miradi 7 ya barabara yenye jumla ya Km. 1,562
inaendelea kufanyiwa upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi. Hiki ni
kielelezo dhahiri cha mafanikio makubwa ambayo yameiweka nchi yetu
katika chati ya kuwa na miundombinu ya kisasa ya barabara. Mwelekeo wa
Sera za serikali yako katika miaka ya 2010 hadi 2020 umeainisha jukumu
kubwa la nchi yetu katika kipindi hiki ni kutekeleza lengo la Dira 2025
la kuleta mapinduzi ya uchumi yatakayoitoa nchi kutoka kwenye dimbwi la
uchumi ulio nyuma na tegemezi na kuiingiza katika mkondo wa uchumi wa
kisasa wa taifa linalojitegemea.
Dhana ya Kujenga Uchumi wa Kisasa inalenga katika modenaizesheni ya uchumi.
Modenaizesheni kimsingi ni kuongeza maarifa na matumizi ya sayansi na teknolojia
katika sekta za uzalishaji. Modenaizesheni ya uchumi inalenga katika kuongeza
uzalishaji, ufanisi na tija katika uchumi hususan katika kilimo, ufugaji, uvuvi na
viwanda.
Mapinduzi ya Kilimo
Kilimo ndio msingi wa uchumi wa kisasa na njia sahihi ya kuutokomeza
umasikini.
Mheshimiwa rais umekuwa muumini wa dhati kwamba kilimo cha kisasa
kinachotumia Kanuni na zana bora za kilimo ndio ufunguo wa maendeleo ya
uchumi wa nchi yetu. Kilimo cha kisasa kina uwezo wa kutoa mazao mengi zaidi
kutoka kila ekari iliyolimwa. Kwa nchi yetu, ziada hiyo ya mazao ina faida kubwa
zifuatazo:-
(a) Kuipatia kila familia, kijiji na Taifa chakula cha kutosha ili kukomesha njaa.
(b) Kulipatia Taifa mavuno mengi ya kuuza ili kupata fedha za kigeni kwa ajili
ya maendeleo ya nchi.
(c) Ziada ya mazao huunda mazingira muafaka ya kuanzishwa viwanda vya
usindikaji na utengenezaji wa bidhaa za viwandani.
(d) Familia yenye ziada ya mazao huutokomeza umaskini kwa kuuza ziada
hiyo kwenye soko na kupata fedha za kujiletea maendeleo.
32. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ya utekelezaji wa Ilani ya mwaka 2005-
2010, Serikali zetu zilichukua hatua kubwa katika kukipatia kilimo mwelekeo wa
kisasa ili kiondokane na zana duni, mashamba madogo, kutozingatia kanuni bora
za kilimo na kuridhika na mavuno ya kujikimu.
Mheshimiwa
Rais, kwa heshima na taadhima tunapenda kukupongeza kwa dhati kwa
kuanzisha mchakato wa Katiba mpya licha ya changamoto zilizojitokeza
katika mchakato huo. Sote tunatambua nia yako ya dhati kuhakikisha taifa
letu linapata katiba mpya kabla hujamaliza awamu yako ya pili ya
uongozi hapo mwakani. Tunakusihi mchakato huu usiwe chanzo cha machafuko
nchini mwetu bali maridhiano ya kisiasa yawe ndio msingi mkuu wa
kupatikana kwa katiba itakayolivusha taifa letu kwa miaka mingi ijayo.
Mwisho tunakutakia safari njema na mafanikio tele katika kutekeleza
majukumu yako.
4. CHANGAMOTO
a) Kushuka kwa thamani ya shilingi
Shilingi
ya Tanzania imekuwa haijatengamaa kwa vipindi tofauti tofauti
ukilinganisha na Dola ya Kimarekani. Hali hii haijawa chachu katika
juhudi za kimaendeleo zinazofanyika. Katika suala la kushuka kwa thamani
ya shilingi, Serikali inatakiwa kujenga uchumi imara uliojengeka kwenye
shilingi iliyoimara ukilinganisha na Dola ya Kimarekani
b) Bajeti isiyotosheleza mahitaji
Bajeti
ya Tanzania imekua isiyojitosheleza hasa kwa kuwa ni bajeti tegemezi.
hii imesasababisha mambo mengi kukwama. wahisani wengi wamekua hawaleti
pesa kwa wakati au kuleta fedha kwa masharti magumu yanaitesa nchi.
Vyanzo vingi vya mapato vimekua visivyotosheleza na hivyo kupelekea
bajeti ya maendeleo kuwa finyu ukilinganisha na mahitaji. Katika
suala hili tunaishauri, Serikali ibuni vyanzo vipya na vya mbadala vya
mapato ili kukusanya fedha ya kutosha itakayotoshereza mahitaji ya
kibajeti
c) Rushwa na ufisadi,
hili
ni tatizo na tishio katika maedeleo ya Tanzania, viongozi wengi katika
sekta mbalimbali Serikalini na hata sekta binafsi wamekuwa si waaminifu
tena. Wamekuwa wakidai rushwa za aina tofauti au kufanya ufisadi,
ubadhirfu wa fedha na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa kasi ya maendeleo
katika sekta mbalimbali.
d) Kushuka kwa uzalendo
Watanzania
wa sasa si wa zamani. Zamani kulikuwa na misingi ya kimaadili na
mafunzo iliyopelekea watanzania wengi kuipenda nchi yao na hivyo
kupelekea kuwa wazalendo. Hali si hivyo tena kwa sasa, hii ni kutokana
na kuibuka kwa changamoto mbalimbali za sayansi na teknolojia hivyo
kumepelekea watu kuwa wabinafsi zaidi kuliko kujali masuala yanayohusu
watanzania kwa jumla.
5. HITIMISHO
Mwisho kabisa mheshimiwa Rais, tunapenda kutoa pongezi zetu za dhati
kwa kutunukiwa nishani mbalimbali kutoka sehemu tofauti duniani ikiwa ni
ishara ya wao kutambua mchango wake baadhi ya nishani hizo ni kama
Nishani Ubora wa Lulu ya Afrika (Bwana tukufu) Julai 2007 Nishani ya
Hilali Kijani ya Komori Machi 2009,Nishani ya Abdulaziz Al Saud ,Aprili
2009,Nishani ya Ubora Novemba 2009 ,Nishani ya Oman , Oktoba 2012
pamoja na tuzo za hivi karibuni za Tuzo la Nyota wa Demokrasia Afrika
2014 – Icon of Democracy Award Winner for 2014 in Africa
Wewe ni kioo kwetu kama vijana na wapiganaji wengine wote, tutakufanya
mwenye tabasamu siku zote kwa kuishi uvumilivu wako wa kisiasa na
kiumbe kinachopenda mwafaka pale maslahiya kitaifa yanapotamalaki.
Wenu Mtiifu,
Loveness Mamuya – Kada Mzalendo CCM Marekani