SUAREZ AANZA NA VIJANA WA BARCELONA B
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/suarez-aanza-na-vijana-wa-barcelona-b.html
Mshambuliaji
kutoka nchini Uruguay Luis Suarez, bado ana hamu ya kuwa sehemu ya
kikosi cha FC Barcelona ambacho kwa msimu huu kipo chini ya meneja
kutoka nchini Hispania Luis Enrique Martínez García.
Suarez,
anaetumikia adhabu ya kufungiwa kucheza soka katika michuano ya
kiushindani kwa kipindi cha miezi minne, ameonyesha hamu ya kutaka
kurejea na kujiunga na wachezaji wengine wa FC Barcelona ambapo itakuwa
ni mara yake ya kwanza baada ya kusajiliwa akitokea Liverpool, kufutia
juhudi anazo zionyesha katika mazoezi pamoja na michezo ya kujipima
nguvu ambayo inakihusisha kikosi cha Barcelona B.
Usiku
wa kuamkia hii leo, mshambuliaji huyo alieacha gumzo nchini Brazil
baada ya kumng’ata beki wa kati wa timu ya taifa ya Italia na klabu ya
Juventus Giorgio Chiellini, alicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya
taifa ya Indonesia chini ya umri wa miaka 19 ambapo Barcelona B
imeichapa Indonesia kwa mabao 6 kwa sifuri.
Kocha
wa Barcelona Luis Enrique amesema alitaka Suarez kucheza mchezo huo ili
kuwa katika hali ya hamasa ya kimchezo, kabla ya kurejea uwanjani rasmi
mwishoni mwa mwezi oktoba.
Suarez
anaruhusiwa kushiriki michezo ya kirafiki pekee, na hatashiriki
michuano ya ligi ya nchini Hispania La Lila mpaka tarehe 24 mwezi oktoba
ambapo Barcelona itakutana na Real Madrid