MTOTO AGONGWA NA GARI NA KUFARIKI IRINGA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/mtoto-agongwa-na-gari-na-kufariki-iringa.html
Mtu mmoja amefariki mkoani Iringa baada ya kugongwa na gari.
Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo kamanda wa jeshi la polisi Mkoani
Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema Kelsensia Bonifasi umri miaka 7
mwanafunzi wa dalasa la kwanza shule ya msingi Sun Academy iliyopo
maeneo ya Isakalilo Manispaa na mkoa wa Iringa amefariki papo hapo baada
ya kugongwa na gari lenye namba za usajili T.306 CRM aina ya toyota
Hiace.
Kamanda Mungi ameongeza kuwa ajali hiyo imetokea katika barabara ya
Iringa-Kalenga Manispaa na Mkoa wa Iringa, chanzo kikiwa ni mwendo kasi
na dereva wa gari hilo Rajabu Adamu umri miaka 28 mkazi wa eneo la
Kihesa Manaispaa ya Iringa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi
zaidi.