Sababu ya Nicki Minaj kuzuiwa kuingia katika shule aliyosoma yawekwa wazi
Ijumaa iliyopita, Nicki Minaj aliandika malalamiko yake kwenye akaunti yake ya Twittter akidai kuwa mkuu mpya wa shule aliyosoma a...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/sababu-ya-nicki-minaj-kuzuiwa-kuingia.html

Ijumaa iliyopita, Nicki Minaj aliandika malalamiko yake kwenye akaunti yake ya Twittter akidai kuwa mkuu mpya wa shule aliyosoma alimzuia kuingia shuleni hapo kuongea na wanafunzi kwa lengo la kuwainspire.
Wengi walidhani kuwa tatizo ni video na picha zisizo na maadili za Nicki Minaj ambazo zilimfanya mwalimu huyo kudhani asingekuwa mfano mzuri kwa wanafunzi wake.
Lakini kwa mujibu wa Mediatakeout, moja kati ya wajumbe wa baraza la wazazi waliweka wazi sababu ya Nicki kunyimwa kibali.
Ameeleza kuwa
Nicki Minaj alilenga katika kutaka kujitangaza zaidi kwa kuwa baada ya
kukatazwa na kitengo cha elimu cha New York kuingia na wapiga picha za
video kwenye shule hiyo.
“Ukweli ni
kwamba Ms. Minaj aliambiwa na kitengo cha elimu cha New York (NYC
Department of Education) kuwa asingeruhusiwa kuingia shuleni pale na
crew ya television. Kitengo hicho kina sera zake kulinda faragha na
usalama wa kila mwanafunzi. Nina uhakika wote tunakubali utekelezwaji
makini wa sera hii kwa kuzingatia usalama wa watoto wetu.
Ameongeza kuwa
Nicki Minaj alitaka kuweka kwenye video kila kitakachofanyika pale kama
sehemu ya kampeni ya kujitangaza kwa umma kwa mazuri anayofanya.