MSIMAMO!! TIMU YAAGA MASHINDANO BAADA YA KUKATAA KUVUA HIJAB KABLA YA MECHI!!!
Timu ya wanawake ya Qatar ya mchezo wa mpira wa kikapu imejiondoa kutoka mashindo ya bara Asia
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/msimamo-timu-yaaga-mashindano-baada-ya.html
Timu
ya wanawake ya Qatar ya mchezo wa mpira wa vikapu imejiondoa kutoka
mashindo ya bara Asia yanayofanyika huko Korea Kusini baada ya kuagizwa
kuvua hijab kabla ya mechi yao dhidi ya timu ya Mongolia .
Wanawake
hao walikataa kata kata kuvua vazi hilo na wakajiondoa mashindanoni
wakidai inakiuka maagizo ya dina ya Kiislamu inayomtaka mwanamke
kujistiri nywele zake haswa akiwa faraghani.
Sheria
za shirika la mchezo huo duniani haziruhusu kuvaliwaj kwa vitambaa vya
kichwani wakati wa mechi lakini sasa wamekuwa wakijadili iwapo sheria
hiyo itaondolewe.
Hata
hivyo ilipowadia wakati wa mechi yao dhidi ya Nepal sheria hiyo haikuwa
imebadilishwa na hivyo iliwabidi kuyaaga mashindano.
Fani nyengine za michezo katika mashindano hayo ya Bara Asia zinaruhusu uvaliwaji wa hijab.
Timu ya taifa ya unyanyuaji uzani ya Iran imekuwa ikishiriki mashindano hayo huku wakiwa wamevalia hijab.
Baraza la mashindano ya Olimpiki ya Bara asia OCA imesema kuwa haki za wachezaji ni zinapaswa kupewa kipaombele .
Baada
ya kuyaaga mashindano hayo mchezaji wa Qatar Amal Mohamed A Mohamed
alisema kuwa walikuwa wamehakikishiwa kuwa wataruhusiwa kushiriki
mashindano hayo wakiwa wamevalia hijab na hivyo hawaelewi kwanini sheria
hiyo haijabadailishwa.
''nina hakika kuwa hatutashiriki mashindano yeyote ya Bara Asia hadi sheria hiyo ibadilishwe''
Mashindano
hayo hufanyika kila baada ya miaka 4 na huwaleta pamoja washiriki 9000
kutoka mataifa 45 yakishindana katika fani 36 ya michezo.
Mashindano hayo yatamalizika tarehe 4 Oktoba.