MANGALA ALMANUSURA AIHARIBIE SIKU MANCHESTER CITY....LAMPARD, DZEKO NI 'HATAREEE'!
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/mangala-almanusura-aiharibie-siku.html
Frank Lampard akipongezwa na Pablo Zabaleta baada ya kuifungia Manchester City bao la nne
MANCHESTER City wamerudi katika njia ya ushindi kufuatia kuibuka na ushindi wa 4-2 ugenini dhidi ya Hull City uwanja wa KC.
Eliaquim Mangala alifanya makosa yaliyowafanya Manchester City wafungwe mabao mawili.
Mabingwa hao wa EPL walipoilipa FC Porto
paundi milioni 32 kumsajili Mangala na kuweka rekodi ya beki ghali
zaidi katika historia ya soka la England, walitaka na malengo ya
kupunguza magoli.
Hata hivyo, Mfaransa huyo amejifunga
goli na kusababisha penalti iliyotia kambani na kupelekea vijana wa
Manuel Pellegrini kufuta magoli mawili waliyokuwa wanaongoza.
Mabao mawili ya kuongoza ya City yalifungwa dakika za mapema na Sergio Aguero na Edin Dzeko.
Lampard alikaa eneo zuri kwa ajili ya kumalizia krosi ya Zabaleta
Edin Dzeko akishangilia baada ya kuifungia Man City goli la tatu dhidi ya Hull City