http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/ligi-kuu-tanzania-20142015-matokeo-ya.html
|
Golikipa
wa Polisi Morogoro, Abdul Ibad akijaribu kuokoa bila mafanikio kiki
iliyopigwa na mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi wakati wa mchezo wa
Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam leo September 27,2014.
Timu
ya soka ya Simba SC imelazimishwa sare ya pili mfululizo katika Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya jioni hii Septemba
27,2014,kufungana bao 1-1 na Polisi Morogoro Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Hiyo
ni sare ya pili mfululizo kwa kocha Mzambia, Patrick Phiri baada ya
wiki iliyopita kutoka 2-2 na Coastal Union Uwanja wa Taifa, licha ya
kuongoza 2-0 hadi mapumziko.
|
|
Mshambuliaji
wa Simba, Emmanuel Okwi akishangilia bao aliloifungia timu yake wakati
wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Polisi ya Morogoro
uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni
Ramadhani Singano 'Messi'
Hadi
mapumziko, tayari Simba SC ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa
na Mganda, Emmanuel Okwi dakika ya 32 akimalizia pasi fupi ya Mohammed
Hussein ‘Tshabalala’.
Timu
ya Polisi inayofundishwa na Mohammed ‘Adoph’ Rishard ilibadilika na
kuanza kusukuma mashambulizi langoni mwa Simba SC ambapo Danny Mrwanda,
mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, aliisawazishia Polisi baada ya
kumzidi mbio na maarifa beki Joseph Owino kabla ya kumchambua vizuri
kipa Hussein Sharrif ‘Cassilas’.
|
Azam
FC imepata ushindi wake wa pili baada ya kuibuka na ushindi wa mabao
2-0 dhidi ya Ruvu Shooting leo kwenye Uwanja wa Chamazi.
Azam
FC ambao walianza ligi kwa kuitwanga Polisi Moro kwa mabao 3-1,
imeshinda mabao hayo mawili leo, yote yakitupiwa kimiani na Mrundi,
Didier Kavumbagu ambaye sasa ana mabao manne.
Matokeo mengine ya Ligi Kuu Vodacom 2014/2015 ni kama ifuatavyo:-
Azam FC 2 - 0 Ruvu Shooting
Mtibwa Sugar 3 – 1 Ndanda FC
Mbeya City 1 – 0 Coast Union
Mgambo Shooting 0 – 1 Stendi United