DKT BILALI AZINDUA Kivuko Kipya cha MV Tegemeo jijini Mwanza
Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa kivuko hicho kipya cha MV Tegeme...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/dkt-bilali-azindua-kivuko-kipya-cha-mv.html
Makamu
wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akibonyeza kitufe kuashiria
uzinduzi rasmi wa kivuko hicho kipya cha MV Tegemeo.
Kivuko
kipya na chakisasa cha MV Tegemeo kama kinavyoonekana, kimetengenezwa kama
mfano wa Meli kutokana na huduma zake.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli
akimuonesha Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal jinsi kivuko kipya cha MV
Tegemeo kitakavyofanya kazi.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Marceline Magesa akimuonesha
Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal baadhi ya sehemu ndani ya
Kivuko hicho kipya.
Makamu
wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwa pamoja na Waziri wa
Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutoka kukagua sehemu ya
kuendeshea kivuko hicho
Makamu
wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi
Dkt. John Pombe Magufuli wakifurahia ngoma iliyokuwa ikichezwa ndani ya kivuko
hicho kipya.
Makamu
wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal kushoto akifurahia jambo na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli
pamoja na Dkt Charles Tizeba kabla ya
uzinduzi wa Kivuko cha MV Tegemeo.
Makamu
wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal kulia akizungumza na Waziri wa
Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiwa njiani ndani ya Kivuko cha MV
Misungwi mara baada ya kumalizika kwa sherehe za ufunguzi wa kivuko kipya cha
MV Tegemeo.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kulia akimsikiliza Mbunge wa Buchosa
na Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba wakati wa Uzinduzi.
Makamu
wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akikata utepe kuashiria
uzinduzi rasmi wa Kivuko kipya cha MV Tegemeo kitakachotoa huduma kati
ya Kahunda hadi kisiwa cha Maisome katika Wilaya ya Sengerema Mkoani
Mwanza. Wengine walioshikilia utepe ni pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt.
John Pombe Magufuli , Mbunge wa Buchosa Dkt Charles Tizeba na Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Ujenzi