UFAHAMU:-Rais Kikwete akikasirika au mtu akimuudhi nyumbani huwa inakuwa hivi….
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/ufahamu-rais-kikwete-akikasirika-au-mtu.html
|
Labda
inawezekana hii ikawa mara yetu ya kwanza kusikia upande wa pili wa
President wetu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete ambae
tumezoea tu kumuona akihutubia, akijumuika na watu mbalimbali kwenye
matukio ya furaha na huzuni lakini kuna mengine hatuyajui kuhusu yeye.
Mtoto
wake Ridhiwani Kikwete ambae ni mbunge wa Chalinze ameongea kwenye
Exclusive na millardayo.com na kueleza ni jinsi gani inavyokua pale
ambapo baba yake anakasirika au anapokasirishwa akiwa nyumbani.
|
|
;‘Jambo
akiwa halitaki mara nyingi hupenda kusema achana na hilo lakini kama ni
mtu kafanya jambo flani sio zuri utamsikia mzee tu anasema huyu mtu
bwana achana nae….. maarifa yake madogo, naweza kutoa ushuhuda mbele za
watu mzee wangu mimi sio mtu ambae ameishi kwenye mazingira yanayotoa
fursa ya matumizi ya lugha ngumungumu kama matusi‘;
;‘Yani
mtu akimuudhi… huwezi kusikia amefikia hatua ya kutamka labda huyu
mshenziiii…. sina kumbukumbu ya mimi kumsikia akitamka neno kama hilo,
mara nyingi ukikosea anasema huyu maarifa yake madogo kwelikweli‘; – Ridhiwani
|