Ubeljiji 2-1 Algeria
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/ubeljiji-2-1-algeria.html
Wachezaji wa akiba, Marouane
Fellaini na Dries Mertens waliisaidia Ubeljiji kupata ushindi muhimu
dhidi ya Algeria katika mechi yao ya ufunguzi wa kombe la dunia huko
Brazil.
Wawili hao walimarisha sifa za Ubelgiji kuwa
moja ya timu bora katika michuano hii ya kombe la dunia, walipofunga
mabao mawili na kuifanya timu yao kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya
timu bora kutoka Afrika; Algeria.Fellaini alifunga bao la kwanza; kwa kichwa katika dakika ya 70.
Mertens naye akafunga la pili dakika kumi baadaye katika dakika ya 80 baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Eden Hazard.
Kevin De Bruyne alichangia vilivyo katika kupatikana kwa mabao yote ya Ubeljiji na bila shaka mkufunzi wa Ubeljiji, Marc Wilmotsatakuwa na kila sababu ya kufurahia alama hizo tatu kutoka kwa mechi ambayo ilionekana kuwa imemponyoka
Hazard na De Bruyne walikuwa na nafasi nyingi, ila safu ya ulinzi wa Algeria uliwazuia kumpitishia mshambulizi Romelu Lukaku mpira.
Madjid Bougherra na Rafik Halliche walilinda eneo la penalti la Algeria na kuyazuia mashambulizi ya wabeljiji .
Kufikia dakika ya 65, Wimots alikua amefanya mabadiliko mengine mawili; Divork Origi aliingia katika nafasi ya Lukaku naye Fellaini akamwingilia Mousa Dembele.
Origi alipata nafasi nzuri pia, mapema baada ya kuingia kwake lakini kipa, M’Bolhi akausimamisha mkwaju wake wa chini.
Wachezaji wa akiba walioingizwa na Wilmots walizidi kushambulia naye Mertens akafunga la pili dakika kumi baadaye.
Hili liliwafanya wabeljiji kutegemea mikwaju ya kutoka mbali kutekeleza mashambulizi yao.
Axel Witsel alimjaribu kipa wa Algeria, Rais M’Bolhi na mkwaju mmoja wa kutoka umbali wa yadi 25.
Timu zote zilipoteza nafasi nzuri kupitia mikwaju ya kona.