MTIFUANO WA UBELGIJI NA ALJERIA, WAAFRIKA HALI BADO TETE KOMBE LA DUNIA BRAZIL
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/mtifuano-wa-ubelgiji-na-aljeria.html
Manywele! Nyota wa Manchester United , Marouane Fellaini akishangilia bao lake la kusawazisha .
Marouane Fellaini akitokea
benchi ameifungia Ubelgiji bao la kusawazisha katika kipindi cha pili
na kuiwezesha nchi yake kupata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wao wa
ufunguzi wa kombe la dunia wa kundi H dhidi ya wawakilishi wengine wa
Afrika, timu ya taifa ya Algeria.
Winga wa Chelsea, Eden
Hazard ndiye aliyetengeneza bao la pili na la ushindi alilofunga Dries Mertens.
Mkombozi: Dries Mertens (kushoto) aliwafungia Ubelgiji bao la ushindi
Beki wa Tottenham, Jan Vertonghen alifanya makosa na kusababisha penati katika kipindi cha kwanza.
Jan Vertonghen akimuangusha mchezaji wa Algeria, Sofiane Feghouli na mwamuzi kutoa penati.
Jan Veryonghen akimlalamikia mwamuzi ,Marco Rodriguezna kwa kutoa penati lakini alipewa onyo ya kadi ya njano.
Sofiane Feghouli akishangilia bao lake la penati.