JOSE MOURINHO AIBUKA NA KUMKANDIA PEPE, ASEMA KWANZA SIO MRENO
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/jose-mourinho-aibuka-na-kumkandia-pepe.html
Pepe alimpiga kichwa Muller wakati Ureno wakiwa nyuma kwa mabao 2-0.
BEKI wa kati , Pepe, aliingia katika malumbano makali na mshambuliaji wa Ujerumani, Thomas Muller na kuambulia kadi nyekundu Ureno ikipoteza mchezo wa kwanza kombe la dunia kwa kipigo cha mabao 4-0.
Baada
ya tukio hilo, Jose Mourinho amechukizwa na kitendo cha pepe na
kumlaumu kuwa yeye ndiye chanzo cha matokeo mabaya kwa Ureno.
Tayari
Ureno walikuwa nyuma kwa mabao 2-0 wakati beki huyo akioneshwa kadi
nyekundu, hata hivyo Mourinho amesema `Pepe kwanza sio Mreno`, kwahiyo
lazima awe na adabu na hakupaswa kumpiga kichwa Muller baada ya
kumchezea vibaya katika mchezo wa jana jumatatu.
Mourinho
amesema hata kama kadi nyekundu ilikuwa kali kwao, Pepe alizaliwa Brazil, hivyo aliheshimu taifa lake la kuazima.
"Nadhani bao la pili ni kosa lake"