MTUMISHI CHA POMBE, CHAKALI!
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/mtumishi-cha-pombe-chakali.html
Tito Akibugia Ulabu kwa Pupa Wakati Akihubiri.
Cha pombe huyo alikuwa gumzo baada ya kutembea katika miji mikubwa tofauti akieneza kile alichokidai kuwa eti ni unabii kwa kuwataka watu kunywa pombe kwani ni tiba ya magonjwa yote. Ndugu Tito, akiwa anabugia ulabu na kuvuta sigara, alionekana mara kadhaa mitaani akipiga makelele kwamba pombe na sigara ni muhimu kwa mkristo kutumia na kutoa shuhuda kwamba yeye mwenyewe amepona ukimwi kwa kunywa pombe.
Inasemekana kwamba mtumishi huyo cha pombe, alifikishwa hospitali baada ya kupatwa na kichaa akiwa amefungwa kamba, hata hivyo aliruhusiwa na madaktari baada ya vipimo kuonyesha hana ugonjwa wowote na ndipo watu waliompeleka hospitali walipoamua kumpeleka kwenye maombi Kibaha.
