Flatnews

MPYA! INAPAKULIWA.




Safari ya Beatrice imekaribia kuiva mara baada ya kuchohcewa  na”WEWE SI WAKAWAIDA”, Nyimbo mpya kabisa iliyotolewa na mwimbaji  Beatrice William inayobeba jina la album yake ya kwanza, ya injili, inayotarajiwa kuzinduliwa mwezi wa nane mwaka huu. Nyimbo hii imekuwa kivutio kikubwa na kuwapa shauku wapenzi wa muziki wa injiri kuisubiri kwa hamu album hiyo mpya.
Beatrice ambaye awali alikuwa kivutio kikubwa katika muziki wa bongo flava hasa baada ya kutamba katika shindano la Bongo Star Search mwaka 2009, aliokoka na kumrudia BWANA mwaka 2012 na kuanza kuimba nyimbo za Injiri.
Tangu alipoaanza kuimba nyimbo za injili, Beatrice amekuwa kivutio kikubwa kwenye matamasha kwa  staili yake tofauti ya uimbaji na ushambulizi wa jukwaa, hali ambaoyo imewafanya watu waisubiri kwa hamu album yake hii.
Kwa kuwa Bwana ameamua kukifanya chombo hiki kipya katika kazi yake, tunaamini album hii itakuwa ni injili tosha kwa wote watakao ipokea.

Post a Comment

emo-but-icon

item