Azma ya kumaliza ubakaji vitani
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/azma-ya-kumaliza-ubakaji-vitani.html

Angelina Jolie kwenye mkutano wa kujadili swala la ubakaji vitani uliofanyika mjini London
Kongamano kuhusu dhuluma ya ubakaji katika mataifa yaliyo katika mizozo ya kivita, imemalizika hii leo jijini London.
Huku mchezaji sinema wa Hollywood Angelina
Jolie, akiwapongeza viongozi mbalimbali wa kiume duniani ambao
wamejiandaa kukabiliana na itikadi za kale zilizopitwa na wakati.Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry kwa upande wake amesema kuwa inawezekana kumaliza kabisa tatizo la ubakaji kama silaha ya vita.
Wajumbe kutoka zaidi ya mataifa mia moja wamekuwa wakijadiliana jinsi ya kukomesha ukatili na ubakaji wakati wa makabiliano ya kivita.
Wameelezewa matukio mbali mbali ya wanawake waliodhulumiwa kimapenzi.
Mwendesha mashitaka wa mahakama ya ICC, Fatou Bensouda aliambia kongamano hilo kuwa walikuwa katika sehemu mpya ya kihistoria
Matendo ya ubakaji yaweza kukomeshwa kwa ushirikiano wa washika dau wote.