Flatnews

KAVUMBAGU, SURE BOY WATUA MAZOEZINI AZAM FC, OMOG KUTIA MAGUU IJUMAA!



Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Juni 18, 2014, saa 3:32 asubuhi
MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc wanaendelea kujiwinda na msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara na ligi ya mabingwa Afrika mwakani.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Kalimangonga Ongala amesema lengo la kuanza mazoezi mapema ni kusuka kikosi chao kwani wanajua kazi iliyopo mbele yao ni kubwa.
“Tunahitaji kutetea ubingwa wetu, tunahitaji kufanya maandalizi mazuri ya ligi ya mabingwa Afrika. Kwa majukumu haya makubwa, tumeamua kuanza mazoezi mapema”.
“Tulianza na wachezaji kama 12 tu, wengine hawajafika. Kuna wachezaji wapo na timu ya taifa na wale `Maproo` wengi hawajafika bado. Kwasasa tunafanya mazoezi mepesi ya kupasha misuli tu, siku chache tutaanza mazoezi mazito rasmi”
“Kocha anatarajia kuja wiki hii, nadhani atakuja na program nzima ya mazoezi”. Alisema Ongala.
Mazoezi hayo ya Azam fc leo yanaenda siku ya tatu tangu kuanza ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa wachezaji.
Wachezaji ambao wameongezeka katika mazoezi hayo ni Abubakari sure Boy, Agrey Moris, Aishi Manula, Saidi Molad pamoja na Didier Kavumbagu.
Mazoezi hayo yanaendelea kwenye uwanja wa Azam comprex uliopo chamazi ambapo kwa sasa wachezaji wanafanya Mazoezi mepesi mepesi ya kulainisha viungo pamoja na umiliki wa Mpira.
Kocha mkuu Mcameroon, Joseph Marios Omog anatarajia kujiunga na kikosi Ijumaa ya wiki hii.

Post a Comment

emo-but-icon

item