SIO MUDA WA KUTUNISHIANA MISULI UCHAGUZI SIMBA, RAGE, MALINZI HAKIKISHENI NGOMA INACHEZWA JUNI 29
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/sio-muda-wa-kutunishiana-misuli.html
Rais Malinzi busara zako zinahitaji kuwafanya Simba wakamilishe uchaguzi wao.
KWA misimu miwili, Wekundu wa Msimbazi wamekosa
nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa barani Afrika kutokana na matokeo
mabaya waliyokuwa wanayapata katika mitanange ya ligi kuu soka Tanzania bara.
Msimu wa 2012/2013, Simba waliishia nafasi ya tatu
na kuipisha Azam fc katika nafasi ya pili na ubingwa kuchukuliwa na watani wake
wa jadi, Dar Young Africans.
Msimu wa 2013/2014, mambo yakawa magumu zaidi na
kushuhudia Simba wakiambulia nafasi ya nne na nafasi ya tatu ikichukuliwa na
Mbeya City fc, huku nafasi ya pili ikitua mikononi mwa Yanga na Ubingwa ukitua
Azam fc.
Kwa kushika nafasi ya tatu na nne katika misimu
miwili si matokeo mazuri kwa klabu ya Simba kutokana na ukongwe wake.
Yawezekana kimpira si nafasi mbaya. Kushika nafasi
ya tatu au nne katika ligi yenye timu 14 si matokeo mabaya, lakini inategemea
ni timu gani imeshika nafasi hiyo.
Kwa timu nyingi za ligi kuu achilia mbali Yanga na
Azam fc, kushika nafasi hizo ni mafanikio makubwa na ndio maana mara nyingi
viongozi wa timu hizo utawasikia mipango yeo ni kushika nafasi ya tatu, nne na ya
tano, lakini kamwe Simba na Yanga hawawezi kuwa na mipango kama hiyo.
Hadhi ya Simba na Yanga ni kuzungumziaa ubingwa
tu. Kutokana na ukongwe wao, uzeofu na kusheheni mashabiki wengi, inakuwa
dhambi kwa timu hizo kushika nafasi ya tatu au nne ambazo hawawezi kuwakilisha
nchi katika michuano ya kimataifa.
Rage alipofikia na Malinzi ndio suluhisho la fukutu za uchaguzi wa Simba sc
Katika kipindi cha miaka miwili, Simba
wameathirika na mambo mengi, lakini makubwa ni mabadiliko ya mara kwa mara ya
benchi la ufundi na uongozi chini ya Ismail Aden Rage kushindwa kuweka umoja
katika klabu.
Msimu wa 2011/2012 alikuwepo kocha Mserbia Milovan
Circovic, baadaye akaja mfaransa Patric Liewig. Akiwa ameshaanza kuijenga Simba
ya vijana na sasa wanaanza kumuelewa, Liewig akaondolewa na kuletwa Abdallah
Kibadeni. Hawa ni walimu watatu tofauti na wana aina yao ya ufundishaji.
Wachezaji ndani ya muda mfupi walijikuta wakilishwa mifumo tofauti. Sasa walishindwa kushika kwa haraka kwasababu wakianza kuzoea kunatokea mabadiliko.
Kibadeni alikuwa ameanza kuwaweka vijana wake vizuri na tuliona Simba ikianza kutambulika na makinda wake, ghafla anatimuliwa na akaletwa Mcroatia Dravko Logarusic; Huyu naye ana mfumo wake.
Kwa mazingira haya, Simba isingeweza kutengamaa kwa haraka na walihitaji muda.
Wachezaji ndani ya muda mfupi walijikuta wakilishwa mifumo tofauti. Sasa walishindwa kushika kwa haraka kwasababu wakianza kuzoea kunatokea mabadiliko.
Kibadeni alikuwa ameanza kuwaweka vijana wake vizuri na tuliona Simba ikianza kutambulika na makinda wake, ghafla anatimuliwa na akaletwa Mcroatia Dravko Logarusic; Huyu naye ana mfumo wake.
Kwa mazingira haya, Simba isingeweza kutengamaa kwa haraka na walihitaji muda.
Pia uongozi wa Rage kwa muda mrefu umekuwa katika
mvutano na kujikuta ukitumia muda mrefu kujibizana kwa maneno na sio kufanya
kazi za klabu.
Yapo megi, lakini haya yanaweza kuwa matatizo makubwa
yaliyowafanya Simba wawe hapo walipo. Lakini neema inaweza kuja kama uchaguzi
mkuu wa juni 29 mwaka huu utafanyika.
Ukiwasikiliza kwa makini wanachama wa Simba, wana
hamu ya kuiona klabu yao inafanya vizuri msimu ujao, na wamechukizwa na
mizengwe iliyogubika uchaguzi wao.
Michael Richard Wambura ndio chanzo cha mvutano uliopo katika uchaguzi wa Simba na hii ilitokea baada ya jina lake kuenguliwa.
Mwishoni mwa wiki Rais wa TFF, Jamal Malinzi
alisimamamisha uchaguzi wa klabu ya Simba akiitaka kamati ya utendaji iliyopo
madarakani kuunda kamati ya maadili hadi ifikapo juni 30. Maamuzi hayo
yalipingwa na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, wakili Damans Ndumbaro akidai
Malinzi hana mamlaka kikatiba kusimamisha uchaguzi na kusema uchaguzi uko
palepale.
Pia wanachama wengi wa Simba waliguswa na maamuzi
hayo na kutoa malalamiko kwa Malinzi wakidai anaihujumu klabu yao.
Ndumabro alitaja mlolongo mrefu wa vifungu vya
katiba vinavyomuondolea Malinzi nguvu ya kusimamisha uchaguzi, lakini
sitavijadili kwasababu si malengo ya makala hii.
Rais wa Simba sc, Ismail Aden Rage baada ya kuona
kama kuna kutunishiana misuli kati ya Ndumbaro na Malinzi, ikamlazimu kutoa
ufafanuzi na kueleza kuwa ameongea na Malinzi na kumwomba uchaguzi ufanyika
juni 29 kama ilivyopangwa.
Rage aliongea kwa busara na kumuangukia Malinzi
kwasababu kubwa moja ambayo ni kwamba; dirisha la usajili limefunguliwa tangu
juni 15 mwaka huu, lakini Simba wamesimama kusajili mpaka wapate viongozi
wapya.
Kutofanyika uchaguzi juni 29 ni kuithiri Simba kwa
kiasi kikubwa. Wanatakiwa kupatikana viongozi haraka iwezekanavyo ili usajili
uendelee.
Ukisikiliza pande zote mbili, kila upande unaongea
yake, lakini mwisho wa siku, mgombea wa Urais aliyeenguliwa, Michael Richard
Wambura ndio chanzo cha yote haya.
Kuenguliwa kwa jina lake ndio kumeleta mizengwe
katika uchaguzi wa Simba, lakini sio muda muafaka wa kuanza kulizungumzia hili.
Ni wazi Wambura aliwahi kufanya makosa katika klabu hiyo ambapo kubwa zaidi ni
kuipeleka Simba mahakamani.
Sheria za FIFA ziko wazi, mambo ya mpira hayatakiwa
kupelekwa mahakama za kawaida. Kisheria Wambura alijiondoa kwenye masuala ya
mpira alipofanya hivyo.
Lakini kuna makosa yaliendelea kufanyika kwa
Wambura kuachwa na viongozi wa Simba akifanya shughuli za klabu ikiwemo kulipa
ada. Kitendo hiki kilimpa nguvu ya kurudishwa kwenye uchaguzi na kamati ya
rufani ya TFF ya Wakili Julius Lugaziya baada ya kuenguliwa. Kumbuka mpaka sasa
ni mjumbe wa kamati ya utendaji iliyopo madarakani.
Cha msingi kwa Rais Malinzi ni kutambua kuwa Simba
inategemea sana busara za TFF ili kufanikisha uchaguzi wake. Kwa walipofika na
mazingira halisi ya sasa, hakuna jinsi ya kuzuia uchaguzi huo.
Ni jambo la faraja kusikia Rage na Malinzi
wamekubaliana uchaguzi ufanyike, na mimi nilitegemea hivyo kwasababu ndio njia
ya kuinusuru Simba kwa sasa.
Simba ni klabu kubwa, inapokuwa mbovu, ladha ya
ligi kuu inapungua kama ilivyo kwa wenzao Yanga. Kuna faida ya kuwa na Yanga na
Simba imara katika ligi.
Misimu miwili mashabiki wa Simba wameumia vya
kutosha, ipo haja ya kuwaacha wafanye uchaguzi ili wasajili vizuri kwa lengo la
kurejesha makali yao.
Huu si muda muafaka wa kuendelea kuandika mvutano
wa Wambura na kamati ya Ndumbaro, Rage na wanachama wa Simba, Kamati ya
uchaguzi na TFF,ni muda muafaka wa kutoa mawazo ya kuwasaidia Simba wafanye
uchaguzi juni 29.
Rais Malinzi wewe ni baba wa mpira wa Tanzania.
Hakuna mtu wa juu zaidi yako TFF. Kwa lugha nyepesi wewe ndio mtu wa mwisho
kama ilivyo kwa rais wa nchi.
Maneno yako yana nguvu sana, jambo la msingi kwako
ambalo ni ushauri wa bure ni kwamba; kila unapofanya maamuzi kumbuka wewe ni
baba, lazima uangalie athari itakayotokea.
Si jambo zuri hata kidogo kuona watu wanakupinga
hadharani ukiwa Rais. Tamko lako linatakiwa kuwa na nguvu, inapotokea
unapingwa, basi kikazi linakushushia heshima.
Sina wasiwasi na utendaji wako, lakini kuna mambo
yanafanyika na watu kuanza kukuwazia vibaya. Kwa mfano kwasasa kuna maneno
mengi yakikuhusisha kumbeba Michael Wambura. Yawezekana sio sahihi, lakini
matendo yanayotokea ndio yanafikisha jambo hili hapa lilipo.
Cha msingi, wape Baraka zote simba, tena bila
kinyongo ili wafanye uchaguzi, bila kufanya hivyo, klabu hii inaweza kuingia
kwenye mgogoro mkubwa.
Simba inagusa maisha ya watu wengi. Ndio maana ni
rahisi watu kuzimia inapofanya vibaya uwanjani,. Hii ni klabu iliyojaa mioyoni
mwa watu. Waacheni wafanye uchaguzi.
Hizo sheria mnazotumia kubishana kufanya maamuzi
ifike wakati sasa uchaguzi ufanyike. Kama mtu hana vigezo aondolewe, lakini
kama ameonewa basi apatiwe msaada wa kisheria.
Nawatakia kila la heri Simba katika uchaguzi wa
juni 29. Ni matumaini yangu baada ya hapo mtasajili kikosi kizuri.