ANGALIA PICHA KIUMBE CHA AJABU KILICHOZALIWA SINGIDA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/angalia-picha-kiumbe-cha-ajabu.html
Mwanamke
mmoja mkazi wa Kintinku, Wilayani Manyoni mkoani Singida
amejikuta akimwaga machozi baada ya kujifungua mtoto mwenye
kichwa cha ajabu ( tepe tepe). Tukio hilo limetokea jana asubuhi katika hospitali ya Kintinku Health Center iliyopo Wilayani Manyoni…..
Akiongea na Mpekuzi
kwa sharti la kutotajwa jina lake kwa madai kuwa yeye si
msemaji wa hospitali hiyo, Mkunga mmoja wa hospitali hiyo
amedai kuwa mama huyo alifikishwa hospitalini hapo akiwa katika
hatua za mwisho kujifungua.“Alifikishwa
hapa akiwa katika hatua za mwisho . Hakuwa na kadi yoyote
ya Clinic kwa kuwa hakuwahi kuhudhuria Clinic tangu abebe
mimba hiyo.
“Pamoja
na kutokuwa na kadi ya Clinic, tulianza kumsaidia kujifungua,
lakini mtoto aliyezaliwa alikuwa ni wa tofauti kidogo na
alikuwa amefariki dunia.Kichwa chake kilikuwa tepetepe na
kimebonyea bonyea.
“Ilikuwa
ni ngumu kwetu kutambua tatizo alilokuwa nalo mama huyo kwa
kuwa hakuwa na kadi yoyote ya Clinic ambayo ingeweza
kutusaidia kujua maendeleo ya mtoto huyo alipokuwa tumboni “,
alisema Mkunga huyo.
Mpekuzi
ilifanya mahojiano na mama huyo ambaye naye alionyesha
kushangazwa na tukio hilo na kusema hajui tatizo lililomfanya
ajifungue mtoto huyo kwa kuwa hakuwahi kusikia maumivu ya aina
yoyote wakati wa ujauzito huo hadi alipofikia hatua ya
kujifungua….
Katika mahojiano hayo, mama huyo alisema kuwa huo ni uzao wake wa 6 na hajawahi hudhuria Clinic