FABREGAS AMLIPUA WENGER …ASEMA ALITAKA KUREJEA ARSENAL LAKINI AKAAMBIWA NAFASI YAKE IMEZIBWA NA OZIL
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/fabregas-amlipua-wenger-asema-alitaka.html
KIUNGO
wa Hispania Cesc Fabregas amemkaanga Arsene Wenger kwa kufichua kuwa
alifanya maongezi na kocha wa Arsenal kabla hajaamua kujiunga na Chelsea
lakini akaambiwa nafasi yake tayari imezibwa na Mesut Ozil.
Arsenal
walikuwa na nafasi ya kwanza ya kumsajili upya mara baada ya mchezaji
wao huyo wa zamani kuamua kuondoka Barcelona, lakini hatimaye Fabregas
akaamumua kujiunga na Chelsea kwa ada ya pauni milioni 30.
Mashabiki
wengi wa Arsenal walicharuka mara baada ya Fabregas kusajiliwa Chelsea
ambapo walitumia mitandao ya kijamii kushinikiza kocha huyo atimuliwe
kwa kupuuzia kumrejesha kikosini kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27.
"Niliongea
na Wenger lakini akaniambia itamuwia vigumu kunipatia nafasi uwanjani
kwa vile Ozil ameziba vema nafasi yangu," alisema Fabregas katika
mkutano wa waandishi wa habari kwenye kambi yao ya Kombe la Dunia.
"Kulikuwa na sehemu nyingi za kwenda na nkaamua kuchagua klabu mbili au tatu zilizo bora, aliongeza kiungo huyo.
"Nikaongea na Jose Mourinho na akasema angependa kuwa nami. Kutoka hapo kila kitu kikaenda kwa haraka
