WEMA AWAGOMBANISHA DIAMOND, PREZZO
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/wema-awagombanisha-diamond-prezzo.html
RAIS wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul
‘Diamond’ yuko ndani ya bifu zito na mwanamuziki kiwango cha juu kutoka
nchini Kenya, Jackson Ngechu Makini ‘Prezzo’ chanzo kikidaiwa ni Miss
Tanzania 2006, Wema Sepetu.
Bifu la wawili hao limekuja kufuatia
madai kwamba, Prezzo amemtundika Diamond kwenye mtandao akimkejeli kwa
kitendo chake cha kurudiana na Wema na kuweka mambo hadharani.
Ilidaiwa kuwa katika maneno yake,
Prezzo alikandia akisema anamshangaa Diamond anatamba kuwa ana mpenzi
supastaa ambaye ni Wema wakati yeye mwenyewe alishaanguka naye.
Madai yanazidi kusema kuwa Prezzo
akaongeza kwa kuandika kwamba, Bongo hakuna mademu masupastaa kwani hata
Jokate (Mwegelo) aliyewahi kutamba naye si lolote kwake.
Msanii huyo anadaiwa alikwenda mbele
zaidi kwa kusema kama ni ustaa anao yeye mwenye pesa zake na si Diamond
ambaye hamfikii kwa lolote.
MASHABIKI WA DIAMOND WAJA JUU
Baada ya kuanika maneno hayo
yaliyoonekana kujaa kejeli, mashabiki wa Diamond walimshukia Prezzo na
kuanza kumnanga kwa kila mtu anavyoweza mwenyewe ndipo akaanza kuhaha
kutaka suluhu kwa Diamond akimuomba meneja wake awakutanishe.
DIAMOND NAYE AWA MBOGO
Akizungumza kwa hasira na paparazi
wetu usiku wa kuamkia Mei 11, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Element
uliopo Masaki jijini Dar es Salaam, Diamond alisema kufuatia matusi hayo
hatarajii kufika kwenye vikao vya usuluhishi na mtu yeyote yule.
“Nimekasirishwa sana na huyu jamaa
(Prezzo) amenitukana kwenye mtandao mimi na demu wangu (Wema) huku
akijua sijawahi hata siku moja kujihusisha na yeye kwa jambo lolote
lile, daa!” alihamaki Diamond.
HASIRA ZOTE HIZO ZIMETOKA WAPI?
Diamond aliyasema hayo baada ya
meneja wa Prezzo aliyejulikana kwa jina moja la Asa kumtaka Mbongo Fleva
huyo wakutane yeye akiwa na Prezzo ili wamalize tofauti zao.
“Meneja wake aliniita eti tukakae
kikao kuyaongea, mimi sioni sababu ya kukutana na Prezzo, yeye ndiye
alianza kunitukana hivyo kama anataka kweli kuelewana na mimi basi
arejee tena mtandaoni akaombe radhi, nitamuona muungwana.
“Unajua katika muziki ni wachache
sana wenye uwezo wa kutumia ustaarabu katika maamuzi yao, wengi
wanaamini kumtusi mtu ndiyo njia pekee ya kupandisha jina au kumfanya
abusti ngoma yake kumbe huwa ni njia mojawapo ya kujishushia heshima
hasa kwa watu wenye busara walio nyuma yake.”
Mkali wa muziki kutoka Kenya, CMB Prezzo.
ANACHOKIAMINI DIAMOND
Akiendelea kuzungumzia ishu hiyo, Diamond alisema anachoamini yeye, Prezzo alifanya vile ili apate kiki kupitia mgongo wake.
“Najua kama alifanya hayo kwa
kufurahisha nafsi yake basi ilisuuzika. Anachotakiwa kukifanya kwa sasa
ni kurudi mtandaoni akaandike mazuri yangu.
“Kwanza mimi sina hata chembe moja ya chuki na yeye ingawa amenioneshea uswahili wa hali ya juu,” alisema Diamond.
WAKUTANA, WAFUNGIANA VIOO
Hivi karibuni, wawili hao walikutana
katika Ukumbi wa Element, Masaki, Dar ambapo Prezzo alikuwa akifanya
shoo lakini walifungiana vioo.
TURUDI NYUMA
Siku za nyuma, iliwahi kuripotiwa na
vyombo mbalimbali vya habari vya Tanzania na Kenya (hasa magazeti)
kuhusu kuwepo kwa uhusiano wa kimapenzi kati ya Wema na Prezzo ambao
ulidumu kwa muda mfupi baada ya Wema kumwagana na Diamond.Chanzo GPL

