DUNIA IMEKWISHA NJEMBA AFUMWA NA DENTI WA KIUME GESTI
ISHARA za mwisho wa dunia? Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Zeb amekula kichapo na kuishia mikononi mwa polisi baada ya kunaswa katika ...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/dunia-imekwisha-njemba-afumwa-na-denti.html
ISHARA za mwisho wa dunia? Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Zeb amekula kichapo na kuishia mikononi mwa polisi baada ya kunaswa katika nyumba ya kulala wageni (gesti) akiwa na dogo wa kiume aliyedaiwa kuwa ni denti wa sekondari.
Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Zeb akiwa amepigw pingu baada ya kunaswa akiwa na mwanafunzi wa kiume gesti.
Aibu hiyo ya karne ilijiri juzi
Jumatatu kwenye gesti hiyo (jina linahifadhiwa) iliyopo maeneo ya
Manzese, Dar ambapo jamaa huyo alikutwa chumbani na denti huyo
aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 14.
Kwa mujibu wa chanzo makini
kilichoitonya Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global
Publishers, njemba huyo amekuwa na ‘katabia kachafu kakuwafanyia
usodoma’ watoto wa kiume.Habari hizo zilidai kuwa ishu hiyo iliwakera
wakazi wa eneo hilo waliokuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu ndipo
wakaamua kumfungia kazi baada ya kudaiwa kuwa na mtoto huyo chumbani
usiku kucha.
Kwa mujibu wa meneja wa gesti hiyo
(aligoma kuta jina) ambaye alitoa ushirikiano wa kutosha kwa OFM, raia
hao walikuwa wakimchunguza njemba huyo kwa muda mrefu kutokana na tabia
ya kulala kwenye gesti hiyo na watoto wa kiume.
“Mwanzo tulifikiri anakuja na vijana
hao kama marafiki zake wa kawaida lakini tukaingiwa na wasiwasi baada ya
kugundua kuwa alikuwa akilala nao kwa kuwabadilisha,” alisema meneja
huyo.
Alidai kwamba Jumapili iliyopita, majira ya saa 3:00 usiku, kijana huyo alitinga tena kwenye gesti hiyo lakini alikuwa peke yake na kupewa chumba kama kawaida.
Alidai kwamba Jumapili iliyopita, majira ya saa 3:00 usiku, kijana huyo alitinga tena kwenye gesti hiyo lakini alikuwa peke yake na kupewa chumba kama kawaida.
“Wahudumu waliniambia kuwa jamaa
amefika tena na amechukua chumba cha juu lakini safari hii alifika peke
yake, ilinishangaza sana kusikia kaja peke yake kwani siyo kawaida yake
so sikuamini,” alieleza meneja huyo.
Alidai kwamba asubuhi ya Jumatatu,
mishale ya saa 4:00, wahudumu walisikia miguno ndani ya chumba
alicholala njemba huyo ndipo wakakifunga kwa nje kisha kuita polisi na
vijana wa OFM ambao walifika eneo la tukio ndani ya ‘dakika sifuri’.
Meneja huyo alisema kuwa hafahamu
njemba huyo alimuingiza kijana huyo muda gani kwani walimuwekea mtego
siku nyingi akawa anachezwa na machale.
Hata hivyo, Jiji la Dar huwa halina
dogo kwani wakazi wa eneo hilo walijazana kwenye gesti hiyo kutaka
kumpiga jamaa huyo lakini polisi walifanikiwa kuwatorosha eneo hilo na
kuwampeleka Kituo cha Polisi cha Magomeni, Dar.
Hadi OFM inang’oa nanga kituoni hapo,
njemba huyo na kijana aliyekutwa naye walikuwa wakiendelea kuhojiwa.
Kujua kilichojiri usikose kufuatilia magazeti ya Global.

