Wanahabari wasisitizwa kufuata sheria za habari zilizopo
Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Dkt. Aboubakar Rajab akitoa hutuba ya ufunguzi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Uta...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/11/wanahabari-wasisitizwa-kufuata-sheria.html
Mkuu
wa Chuo cha Habari Zanzibar Dkt. Aboubakar Rajab akitoa hutuba ya
ufunguzi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii
na Michezo Zanzibar Ally Mwinyikai katika Mkutano Mkuu wa Wadau wa
Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) uliofanyika ukumbi wa
Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar ambapo alisitiza wanahabari
kuzingatia maadili ya kazi zao. Kulia ni Katibu wa Tume ya Utangazaji
Zanzibar Chande Omar na kushoto ni Mwenyekiti wa ZPC Abdallah Mfaume.
Katibu wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Chande akitoa Mada ya umuhimu wa kuzingatia Maadili kwa Wanahabari katika fani yao.
Mkulima kutoka
kikundi cha Ushirika cha Bambi Mwaka Saburi akichangia katika Mkutano wa
Wadau wa ZPC uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini
Zanzibar ambapo alishauri Wanahabari kuandika zaidi habari za Vijijini
bada ya mijini pekee.
Katibu
wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) Faki Mjaka akisoma
maazimio ya Mkutano wa Wadau wa ZPC uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya
Zanzibar Ocean mjini Zanzibar.
Baadhi ya
Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Zanzibar Press Club ZPC wakiwa katika
Picha ya pamoja na Mgeni rasmi wa Mkutano huo Dkt. Aboubakar Rajab
wakatikati waliokaa huko Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar. Picha
na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
Na Maelezo Zanzibar-21/11/2015
Wanahabari
wametakiwa kuendelea kutii Sheria zilizopo zinazoongoza mwenendo wa
utoaji wa habari nchini, huku Taasisi za kihabari zikiendelea kufuatilia
upatikanaji wa sheria Bora za habari zinazoendana na wakati uliopo.
Hayo yameelezwa
na Katibu wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Chande Omar alipokuwa
akiwasilisha Mada katika Mkutano Mkuu wa Wadau wa Jumuiya ya Waandishi
wa Habari Zanzibar ZPC uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean
mjini Zanzibar.
Amesema licha ya
kuwepo kwa baadhi ya Sheria za habari zilizopitwa na wakati, ni vyema
Wanahabari kuziheshimu na kuzitii huku juhudi mbalimbali zikifanywa na
Wadau kuondoa Sheria hizo.
Chande
amefahamisha kuwa Taasisi kama Vile Baraza la Habari Tanzania, Tume ya
Utangazaji na Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar ZPC ni miongoni
mwa Taasisi ambazo zinafanya kazi za kuwepo kwa Sheria zinaendana na
wakati kwa maslahi mapana ya Taifa.
Aidha katika
Mkutano huo uliojumuisha Washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali
na Binafsi maazimio mbalimbali yalipitishwa ikiwemo Wamiliki wa Vyombo
vya Habari na Waaandishi kwa ujumla kuzingatia Weledi katika utekelezaji
wa majukumu yao.
Azimio jingine ni
kuhakikisha kuwa Taasisi kama Vile Baraza la Habari Tanzania, Tume ya
Utangazaji na Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar ZPC zinashiriki
kikamilifu katika kuhamasisha upatikanaji wa Maslahi bora kwa Wanahabari
ili kuwaepusha kupokea Zawadi kutoka Vyanzo vya habari ambazo hupelekea
kukiuka maadili yao.
Aidha wameazimia kujiepusha na Ushabiki wa Kisiasa ili kuepuka upendeleo wa habari wanazojitoa kwa jamii.
Mmoja wa
Wachangiaji kutoka Jumuiya ya Wakulima Mpwapwa amewaomba Waandishi wa
habari kuandika pia habari za watu wa shamba badala ya kuandika habari
zinazohusu watu wa mijini pekee.
Ametoa mfano
kwamba katika uchaguzi Mkuu uliopita habari zilizoandikwa zilihusu Watu
wa Mijini ambapo kwa upande wa Vijijini Waandishi walishindwa kuonekana
kwenda kuchukua habari.
Hata hivyo
Washiriki wa Mkutano huo pia Waliafiki wazo hilo na kuazimia kufanya
kazi kizalendo na kushirikisha makundi yote ya kijamii ikiwemo kuandika
habari za Vijijini ili kuibua Fursa na changamoto zinazowakabili.
Akitoa hutuba ya
Ufunguzi Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Dkt. Aboubakar Rajab kwa niaba
ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar
Ally Mwinyikai alisisitiza wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao
ili waheshimike katika jamii.
Amesema kukosekana kwa Maadili ya Habari hupelekea Migogoro mingi ikiwemo kuzalisha chuki na fitna miongoni mwa jamii husika.
Jumuiya ya
Waandishi wa Habari Zanzibar hufanya Mkutano Mkuu wa Wadau wake kila
mwaka na kujadili mada kulingana na wakati husika ambapo katika Mkutano
huo Walijadili umuhimu wa Waandishi kuzingatia Maadili katika kupatikana
uchaguzi huru na Wahaki.