Wanafunzi wenye mahitaji maalum vyuo vikuu waaswa kutumia vyema utaalamu walioupata kuendesha maisha yao
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Balozi Nicholas Kuhanga (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wahi...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/11/wanafunzi-wenye-mahitaji-maalum-vyuo.html
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam Balozi Nicholas Kuhanga (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha
ya pamoja na Wahitimu Bora wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es
Salaam (DUCE) wakati wa Mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika
jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Chuo Kikuu Kishiriki cha
Elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa William Anangisye, Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Lwekaza Mukandara na Mwenyekiti wa
Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Bw. Peter Kuhanga. Picha na Frank Shija, MAELEZO
Baadhi ya
wahitimu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE)
wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo hicho
yaliyofanyika chuoni hapo jana.
Kaimu Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ,Balozi Nicholas Kuhanga
akiwatunuku Shahada wahitimu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es
Salaam (DUCE) (hawapo pichani) alipokuwa mgeni wa Chuo katika Mahafali
ya nane ya chuo hicho jana jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Bw. Peter Ngumbulu.
Muhitimu wa
mwaka wa tatu ambaye ameongoza kwa ufauli kwa kupata GPA ya 4.8 Bi.
Ummul Kheir Mustafa akipongezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (UDSM) Bw. Peter Ngumbulu mara baada ya kupokea zawadi
yake ikiwemo kukabidhiwa Cheti chake mbele ya hadhara wakati wa
Mahafali ya nane ya chuo hicho jana jijini Dar es Salaam. Muhitimu huyo
amekuwa mwanafunzi wa kwanza kunufaika na mpango wa chuo hicho wa kutoa
fursa ya kuajiriwa chuoni hapo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katka
masomo yao ikiwa ni njia ya kukabiliana na uhaba wa wanataaluma chuo
hapo.
Muhitimu wa
mwaka wa tatu ambaye ameongoza kwa ufauli kwakupata GPA ya 4.8 Bi. Ummul
Kheir Mustafa akionyesha Cheti chake cmbele ya hadhara mara baada ya
kuwa muhitimu wa kwanza kukabidhiwa cheti wakati wa Mahafali ya nane ya
chuo hicho jana jijini Dar es Salaam. Mbali na kukabidhiwa Cheti chake
cha Shahada papo hapo muhitimu huyo amekuwa mwanafunzi wa kwanza
kunufaika na mpango wa chuo hicho wa kutoa fursa ya kuajiriwa chuoni
hapo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katka masomo yao ikiwa ni njia ya
kukabiliana na uhaba wa wanataaluma chuo hapo.
Mgeni rasmi
wa Mahafali ya nane ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaama
(DUCE) Profesa Martha Qorro akizungumza wakati wa Mahafali hayo
yaliyofanyika jana chuoni hapo. Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu
1156 walitunukiwa Shahada na Stashahada za juu.
………………………………………………………………………………………………..
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Wanafunzi wenye mahitaji maalum
wanaosoma vyuo vikuu nchini wameaswa kutumia elimu wanayoipata
kuendesha maisha yao ili waweze kujiletea maendeleo yao na taifa kwa
ujumla.
Hayo yamesemwa na Prof.
Mshiriki wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Kituo cha Studi za Mawasiliano
Martha Qorro ambaye alikuwa Mgeni Mashuhuri wakati wa Mahafali ya nane
ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaama (DUCE) yaliyofanyika
mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaaam.
Prof. Qorro alisema kuwa mwamko
wa wanafunzi wenye mahitaji maalum kujiunga na elimu ya juu nchini ni
mzuri licha ya changamoto zinazowakumba wanafunzi hao wanapokuwa chuoni.
“Hawa ni wanafunzi wenye uelewa
mzuri wakipata mahitaji yao ya lazima yakiwemo fimbo nyeupe, vifaa vya
kuandikia kwa kutumia nukta nundu, baiskeli za miguu mitatu, viti maalu
na mahitaji mengine ya kijamii” alisema Prof.Qorro.
Prof.Qorro aliongeza kuwa ni
wajibu wa vyuo vikuu nchini kikiwepo Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar
es Salaam kuwasisitiza kwa kuwauliza wanafunzi wanapojaza fomu za
kujiunga waoneshe kuwa wanamahitaji maalum ili waandaliwe mahitaji hayo
ikiwemo usafiri wa bajaji ndani ya chuo ili kuwawezesha kuwahi vipindi
vyao katika maeneo mbalimbali ndani ya chuo.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo
Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa William Anganisye
alipokuwa akitoa taarifa fupi kuhusu mafanikio chuo wakati wa Mahafali
hayo alisema kuwa chuo hicho kimetimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake
ambapo hadi sasa wamehitimu wanafunzi zaidi ya 8000 na jumla ya wahitimu
1156 walitunukiwa Shahada na Stashahada za juu katika mahafali hiyo ya
nane.
Naye muhitim wa mwaka wa tatu
katika ngazi ya shahada ya ualimu katika masomo ya sanaa Andrea Sanga
ambaye pia ni mwanafunzi mwenye mahitaji maalum (mlemavu asiyeona)
alisema kuwa mafanikio yake katika masomo yametokana na kuheshimu ratiba
kuu ya masomo chuoni hapo pamoja na ratiba yake binafsi ya kujisomea.
Zaidi ya hayo, Sanga alisema
kuwa maktaba ya chuo, ushirikiano mzuri kati yake na wanafunzi wenzake
na walimu wake, kuhudhuria semina na kufanya kazi kwa wakati na
kupunguza msongamano wa kazi nyingine ndiyo vimekuwa dira yake kuu ya
mafanikio.