Flatnews

TUANZIE WAPI ILI KUWAPATA SAMATTA, ULIMWENGU, KWA AJILI YA TAIFA STARS YA KESHO?

Habari zenu wanajamii wa kitanzania hasa wale wapenda soka. Nimekaa nikafikiri sana na kupata muarobaini ambao ukitumika ipasavyo kwa mi...


Habari zenu wanajamii wa kitanzania hasa wale wapenda soka. Nimekaa nikafikiri sana na kupata muarobaini ambao ukitumika ipasavyo kwa mipango madhubuti basi tunaweza kulikaribia lengo au kulifikia lengo kabisa katika kupiga hatua ya kuzalisha vipaji madhubuti vya soka.

TFF ndiyo iliyopewa dhamana ya kusimamia soka pamoja na kutoa dira ya muda mfupi na muda mrefu ya muelekeo wa soka la faifa letu.
Kwa mipango ya muda mfupi, TFF inatakiwa kuweka sheria kali kwa kila club inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania kuwa na timu mbili za vijana nikimaanisha U17 pamoja na U21.
Hii itasaidia kuzalisha vipaji endelevu kila kukicha na kuzipunguzia timu gharama ya kusajili wachezaji kwabei ghali, badala yake hizo gharama kuelekezwa kwa timu hizo za vijana kupata vifaa na elimu ya kuwa professional kwenye kazi hii ya mpira.
Pia ili kuona timu hizi za vijana zinakuwa active na sio jina tu, TFF waandae ligi kuuza za U17 na U21 ambazo zitashirikisha timu ambazo timu kubwa zao zipo ligi kuu. Tunaona mataifa yaliyoendelea kama Uingereza, Spain na Germany wamefanikiwa sana kwenye hili na kufanya nchi hizo kupiga hatua kisoka.
Pia ligi hizi za vijana zikiwa zinafanyika zitampa wasaa mzuri kocha wa vijana kuona vipaji na kuchagua wachezaji kwa ajili ya timu za taifa za vijana ambazo ndiyo zitakuwa zalisho bora kwa senior national team.
Kwakweli watanzania wenzangu zoezi hili likifanyika kwa ufasaha kabisa ni lazima tutawapata akina Samata wengi sana, pia vijana wakiwekwa kwenye timu wakiwa wadogo hata nidhamu ya uwanjani na ya nje ya uwanja itakuwa ni rahisi kufundishwa na kuweza kukua nayo kuliko kuanza kuwafundisha wakiwa wakubwa tayari, siri kubwa ya wachezaji kufanikiwa ni nidhamu binafsi ya nje na ndani ya uwanja.
Pia vilabu vitapata faida pale wanapopata majeruhi wengi kwenye clubs zao, watakuwa na uwezo wa kuchukua vijana wao na kuwatumia kwenye ligi mara moja (Kama sheria ya TFF inaruhusu).
Kwa mipango ya muda mrefu TFF kama chombo kilichopewa dhamana ya kusimamia soka nchini wanatakiwa waje na mipango madhubuti ya kuweza kutuvusha, na mojawapo ni kuzalisha wakufunzi wengi wa soka ambao watasambazwa nchi nzima kufundisha vijana wadogo kabisa.
Hii itafanyikaje ilhali tuna Accademy chache nchini? Kwa kuanzia inabidi tuanzie mashuleni kuanzia shule za msingi, kila shule ya msingi inatakiwa iwe na mwalimu aliyesomea mpira na siyo yule anayeangalia tu na kuja na mambo yake ambayo hayana program.
Kwahiyo TFF kwa kushirikiana na serikali wanatakiwa waweke mwalimu wa soka kwa kila shule ya msingi anayepata nafasi ya kufundisha soka na nidhamu kuanzia umri mdogo mashuleni (Wizara ya Elimu na michezo ni wadau wakubwa kwenye hili). Lakini sio kwa kuishia hapo tu pia kwa ngazi ya shule za secondary waalimu wa soka wanahitajika pia.
Kumbuka hii ni mipango ya muda mrefu siyo ya muda mfupi kwahiyo matunda yake tutaanza yaona baada ya miaka 10+, tunatakiwa tuwe wavumilivu sana ikiwa tunataka kuvuka hapa tulipo angalau tukipata waalimu wa soka kama1000 utakuwa ni mwanzo mzuri sana kwa maendeleo ya soka la nchi yetu kwa miaka 10+ ijayo. Na wakufunzi hao wanatakiwa wawe na agenda moja ya taifa na sio kila mmoja kuwa na program yake, lengo liwe moja nchi nzima (Germany wamefanikiwa sana kwa hili tunaweza kuwatumia kama case study).
Lakini tukiwa tunatumia hizi shule zetu za kawaida hapohapo TFF inatakiwa iweke vipaombele kwenye kujenga Academy zake na pia kuviwekea vilabu vya soka masharti ya kushiriki ligi kuu ikiwa ni pamoja na kuwa na Academy inayoeleweka ndani ya miaka 10 ijayo (Tuliona mpango wa Sunderland kutaka kuisaidia Simba ila hatujui ulipofia mpango huo).
Timu kama Azam imefanikiwa kwa hilo chini ya miaka 10 basi hata hawa wengine wakiwekewa masharti hayo wanaweza kufanya.
Kila jambo lolote zuri linahitaji gharama kwahiyo wasimamizi wa mpira wanatakiwa wafanye plan nzuri na kuandaa budget yenye tija kwa kushirikiana na serikali waweze kutekeleza haya na kutafuta wafadhili wenye nia ya kuibua vipaji nchini ambao najua wapo wengi tu watu wenye nia njema na soka la taifa hili.
Tukumbuke pia uki-invest sehemu kwa pesa nyingi pia outcome yake huwa inakuwa kubwa kama ukisimamia vizuri. Football ni biashara kubwa sana kwa nchi za wenzetu na inachangia asilimia kubwa sana ya pato la taifa kwa nchi hizo.
Ndugu zangu watanzania, wazungu wanasema “this is not a rocket science” na hakuna shortcut kwenye hili lazima tufate procedure na kupata wataalamu wazawa wa kusimamia haya kwa ukamilifu.
Tuache majungu na kuishi kwa mazoea kwamba tutafanikiwa, maamuzi magumu ni lazima yafanyike ili tuvuke. Tutaendelea kwenye makala nyingine kwa kuona mifano hai ya nchi zilizopiga hatua walifanyaje.

Related

SPORTS 8165458455820588618

Post a Comment

emo-but-icon

item