Flatnews

Serikali yatangaza siku 3 za bomoa bomoa Kinondoni

                          Bomoa Bomoa kuanza leo jijini Dar es salaam. S...



                          Bomoa Bomoa kuanza leo jijini Dar es salaam.
Bomoa Bomoa kuanza leo jijini Dar es salaam.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kupitia Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, inakusudia kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi kwa tatu mbili mfululizo.

Maeneo yaliyotengwa mijini kwa matumizi ya umma ikiwa ni pamoja na maeneo ya wazi, njia za miundombinu na huduma nyinginezo za umma, mara kwa mara hutumiwa vibaya au kuvamiwa na waendelezaji binafsi hivyo kuukosesha umma manufaa yaliyokusudiwa.
Ubomoaji huo untokana na Tamko Na. 6.6.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:
  1. Serikali itahakikisha kwamba maeneo yote mijini yaliyotengwa kwa shughuli za umma yanatumika kwa shughuli zilizokusudiwa na yanalindwa ili yasivamiwe.
Tamko Na. 8.2.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:
  1. Serikali za mitaa zitawajibika kushirikiana na Wizara ya Ardhi kuhakikisha usimamizi mzuri wa ardhi katika maeneo yao.
<a href='https://mpakasi.com/ads/www/delivery/ck.php?n=a08724c9&cb=Math.random()' target='_blank'><img src='https://mpakasi.com/ads/www/delivery/avw.php?zoneid=19&source=https%3A%2F%2Fmpakasi.com&cb=Math.random()&n=a08724c9' border='0' alt='' /></a>
Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Ardhi imebainisha sababu inayopelekea Wizara kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni kuendesha zoezi hili la ubomoaji.
Ubomoaji huu utahusisha nyumba zote zilizojengwa
  1. a)     Bila kibali cha ujenzi
  2. b)     Bila kufuata michoro ya mipango miji
  3. c)      Bila kufuata matumizi ya ardhi (maeneo ya wazi)
Zoezi hili la ubomoaji litaendeshwa na Manispaa ya kinondoni na Wizara ya Ardhi itasimamia sera za ardhi na taratibu za uendelezaji kuhakikisha zinafuatwa na kila mmiliki wa ardhi.
Maeneo ambayo ujenzi wake umekiuka matumizi kusudiwa na yatahusika na ubomoaji huu ni  Mbezi, Tegeta, Bunju, Mwenge na Kinondoni – Biafra. Kazi hii inatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia jumatano tarehe 18/11/2015 hadi ijumaa tarehe 20/11/2015.

Related

NEWS 7011905666338295729

Post a Comment

emo-but-icon

item