Flatnews

Rais Magufuli Atwishwa Zigo la Katiba

JUKWAA la Katiba Tanzania (Jukata) limeitaka Serikali ya Awamu ya Tano kuanza kazi ya kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya.



JUKWAA la Katiba Tanzania (Jukata) limeitaka Serikali ya Awamu ya Tano kuanza kazi ya kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya.

Ni kutokana na serikali ya Rais Jakaya Kikwete iliyokoma Mei 5 mwaka huu baada ya Dk. Magufuli kuapishwa, kura ya maoni ilipangwa kufanyika Aprili 30 mwaka huu lakini haikufanyika.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba amesema kuwa, kushindwa kupatikana kwa Katiba ndani ya muda kulizua hofu kwamba mchakato huo ungeweza kukwama.

“Kama Jukwaa tumeendelea kufuatilia kwa ukaribu, kutafiti na kushauriana juu ya mchakato ulipofikia na namna ya kutoka hapo kama taifa katika kipindi chote tangu mchakato uliposimama,” amesema Kibamba.

Kibamba amesema kwamba, baada ya kushindikana kwa jaribio la kuunganisha kura ya maoni na uchaguzi mkuu, kuna taarifa kuwa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) kwa sasa inaanza maandalizi ya kuitisha upya kura ya maoni ili Watanzania waweze kuipigia kura ya ndiyo au hapana.

Aidha, mchakato wa Katiba Mpya ulianza mwaka 2011 ambapo ulitarajia kukamilika kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambapo serikali ilitaja kuwa Aprili 26 2014 kama siku ambayo katiba mpya ingepatikana.

Amesema, hata baada ya kushindikana, lengo la serikali lilibaki kuwa kura ya maoni juu ya katiba iliyopendelezwa ifanyike Aprili 30 mwaka huu. Hata hivyo, tarehe hiyo ilipita bila kura ya maoni kufanyika.

“Kwa tathimini ya JUKATA , mchakato wa katiba ulianza vizuri hadi kufikia rasimu ya pili ya katiba (Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ) lakini kutekwa kwa mchakato wa katiba wakati wa bunge maalum ilikuwa mwanzo wa kufifia kwa hamasa ya mchakato wa katiba,” amesema Kibamba.

Hata hivyo, kwa kuwa mchakato wa kuandika katiba mpya ulianzishwa na Rais wa Awamu ya Nne, Kikwete na haukukamilika, hivyo JUKATA limemtaka Rais Magufuli baada ya kuunda Baraza la Mawaziri.

Mbali na hilo, JUKATA limesema kuwa limesikitishwa na kitendo cha Jeshi la Polisi kuvamiwa na kuwakamata waangalizi wa uchaguzi wa mwamvuli wa Asasi za Kiraia zinazoangalia uchaguzi ukijulikana kama TACCEO ambao walikamatwa Oktoba 29 mwaka huu.

Pia JUKATA limelaani vikali mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo ambaye pia alikuwa mgombea wa ubunge katika uchaguzi uliopita.

Related

NEWS 1463534805872109783

Post a Comment

emo-but-icon

item