Flatnews

Lembeli aikana Twita ‘inayomshambulia’ Rais Magufuli

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya ya ardhi maliasili na mazingira Bw. James Lembeli...





Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya ya ardhi maliasili na mazingira Bw. James Lembeli
Mbunge mstaafu wa Jimbo la Kahama mkoani Shinyanga James Lembeli ameikana akaunti katika mtandao wa Twita inayodaiwa kumshambulia Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

Akihojiwa kuhusiana na akaunti hiyo iliyotoa ujumbe mwingine hivi karibuni Lembeli amekanusha vikali kumiliki akaunti hiyo akidai kwamba inatumiwa  na watu wenye nia mbaya na yeye kutoa taarifa za uchochezi na uchonganishi.
Amesisitiza kuwa  taarifa zote zinazotolewa kupitia akaunti hiyo yenye jina la James Lembeli na picha yake akiwa na aliyekuwa mgombea urais wa Chadema kupitia mwavuli wa UKAWA Edward Lowassa ni za uongo.
Katika hatua nyingine  Lembeli ameshindwa kutetea kiti chake cha ubunge katika uchaguzi mkuu uliopita ambapo jimbo alilokuwa analitete la Kahama mjini  limechukuliwa na Bw.  Jumanne Kishimba. Moja ya ujumbe katika akaounti hiyo.

Related

NEWS 6514927455476428201

Post a Comment

emo-but-icon

item