Flatnews

Kujitangaza mshindi,Maalim Seif adai yupo tayari kukamatwa

Mgombea Uraisi wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na ...



Mgombea Uraisi wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na Waandishi wa Habari.
Katibu mkuu  wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad kufuatia kujitangaza mshindi wa Urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 amesema yupo tayari kufikishwa mahakamani kwa kitendo hicho  ikiwa ni kosa.

Akizungumza na viongozi wa majimbo, makatibu wa matawi, wajumbe wa mkutano mkuu, wajumbe wa kamati za utendaji za ngazi zote na watendaji wa chama hicho Seif amesema haoni hatua yake ya kuitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imtangaze kuwa mshindi haina matatizo kwa kuwa ana uhakika kuwa ndiye aliyeshinda kwenye uchaguzi.
“Nilichosema ni ZEC initangaze kwa kuwa nilishinda uchaguzi. Je, hapo kuna ubaya gani ati? Nishitakini basi, nasema niko tayari, nishtakini. Alisema Maalim Seif
Katika uchaguzi mkuu uliofutwa Maalim Seif aliwania urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), akichuana vikali na mgombea wa CCM, Dk Mohamed Shein. Kwa upande mwingine,Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) hadi sasa haijamtangaza mshindi na badala yake imefuta matokeo ya kura za nafasi hiyo pamoja na za uchaguzi wa wawakilishi, ikisema uchaguzi utarudiwa tena ndani ya siku 30.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa ZEC Bw.Jecha Salum alibainisha kuwa uchaguzi huo umefutwa kutokana na kasoro kadhaa ikiwemo kuwa na ongezeko la wapiga kura tofauti na walio jiandikisha.

Related

NEWS 2623045883349794913

Post a Comment

emo-but-icon

item