KIMENUKA CCM:..VURUGU KUBWA YAZUKA CCM WABUNGE HAWA WASHIKANA VIKALI KISA NI UNAIBU SPIKA
Vita ya Unaibu Spika ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imefikia patamu baada ya idadi ya wanacham...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/11/kimenuka-ccmvurugu-kubwa-yazuka-ccm.html
Vita ya Unaibu Spika ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imefikia patamu baada ya idadi ya wanachama watano kuchukua na kurejesha fomu za kuomba ridhaa ya kugombea nafasi hiyo.
Jana chama hicho kilitangaza majina ya wanachama watano walioomba nafasi
hiyo na utaratibu wa kupitisha majina matatu ya wabunge wake kwa ajili
ya kupitisha jina moja.
Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa CCM, kitakutana na kupitisha
jina la mgombea wa nafasi ya Naibu Spika, wa Bunge la 11, na baadaye
majina matatu kupelekwa kwa wabunge wa chama hicho kwa ajili ya kupigiwa
kura.
Hadi jana jioni wabunge watano walikuwa wamerudisha fomu za kuwania
nafasi hiyo, na jana usiku kamati na wabunge wa CCM ilikutana kupitisha
jina moja la mbunge atakayepambana na wagombea wa vyama vingine.
Waliochukua fomu ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu; Mbunge wa
kuteuliwa, Dk. Tulia Ackson; Mbunge wa Donge, Sadifa Juma Khalifa;
Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Kisangi na Bahati Ali Abeid.
Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM,
Jenister Mhagama, alisema kikao cha kwanza cha kuchuja majina hayo na
kubakiwa na matatu ni cha Kamati ya Uongozi.
“Leo (jana) usiku kikao cha Kamati ya Uongozi ya wabunge wa CCM
kitafanyika na kutoa majina matatu ambayo yatapelekwa katika kikao cha
wabunge wote katika ofisi za chama, ambao watatoa jina moja la kwenda
kuwania nafasi ya Naibu Spika,” alisema.
Alisema Naibu Spika anatarajiwa kuchaguliwa leo, baada ya kumalizika
uchaguzi wa Spika ambao mgombea wa CCM, Job Ndugai, kushinda kwa
asilimia 70 ya kura katika uchaguzi uliofanyika jana.
SAKAYA KUWAKILISHA UKAWA
Wakati CCM ikitarajia kutoa jina la mgombea Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) unaoundwa na vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema, NLD na CUF,
wametoa jina la Mbunge wa jimbo la Kaliua, Magdalena Sakaya (CUF).
MPAMBANO
Vita katika nafasi ya Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano
imeanza kujitokeza, baada ya baadhi ya vigogo wa CCM, kutolikubali jina
la Mbunge Mteule wa Ilala, Mussa Azzan Zungu.
Vyanzo vya uhakika kutoka ndani ya CCM ambavyo havikutaka kutajwa
majina, vinaeleza kuwa wabunge wengi wa CCM wanamtaka Zungu kushika
nafasi hiyo, lakini kumekuwapo na shinikizo kutoka ngazi ya juu kutaka
kuondolewa jina lake.
“Sisi tunataka Zungu, lakini tunaona dalili za wazi na jitihada za mtu
kuandaliwa kushika nafasi hiyo, ni wazi kuwa watatugawa na watasababisha
nafasi hiyo kwenda upinzani,” alisema Mbunge mteule mmoja ambaye
hakutaka kutajwa jina.
Alisema kiuhalisia hadi jana jina la Zungu ndilo lilikuwa linaaminika
ndilo chaguo la wabunge, lakini hali ilibadilika jana asubuhi na
kuwafanya wabunge kuchanganyikiwa.
“Tunaona kila dalili za mmoja wa wagombea kuandaliwa kushika nafasi
hii, ndiyo maana tunaona mambo yanakwenda haraka haraka,” alibainisha.
NDUGAI NA ZUNGU
Mwanzoni mwa wiki iliyopita Ndugai alipokweda kuchukua fomu, baada ya
kuzungumza na waandishi wa habari, katibu wake aliwataka waandishi
kutoka nje kwa kuwa ana mazungumzo mafupi na Zungu.
Walizungumza kwa dakika 10, ndipo Zungu alitoka na alikataa kuzungumza
na waandishi wa habari na kesho yake alikwenda kuchukua fomu ya naibu
spika.
Inaelezwa kuwa chaguo cha Ndugai ni Zungu kuwa naibu wake, lakini wapo
baadhi ya vogogo wa CCM wanaopinga jambo hilo na kkumtaka mgombea mmoja
kucukua nafasi hiyo.
CHANZO: NIPASHE